Mkuu, Chabusalu, Kwanza asante Kwa uchambuzi wako
Uchambuzi wako huu kwangu Mimi naweza kuuita ni uchambuzi usiokuwa na kiini cha kuonyesha udhaifu wa umarufu wa JPm ama pengine unayonia ya kutaka kuonesha udhaifu wa umatufu wa Magufuli Ila umeshindwa, eidher Kwa yeye amekuibia hoja zote ambazo ungeweza kuxibainisha hapa,
Ni kweli, Kwa temu hii ukiambiwa uoneshe udhaifu wa Magufuli, na serikali yake, kinyume na serikali zilizopita ambazo takribani kila eneo zilikuwa zimepwaya vibaya, usipotaja Neno Democrasia pekee, unaweza Anza kutafuta madhaifu mengine Kwa tochi
Ngoja nikurudishe nyuma, uchaguzi wa 2015 ndio ulikuwa uchaguzi mgumu kuliko chaguzi zote zilizowahi fanyika nchini mwetu Chini ya vyama vingi nchini
Sio Siri, Baada tu ya Mh E.lowassa kuondolewa kwenye kinyang'lo cha kugombea Uraisi, CCM iligawika makundimakundi hata kabla E.lowassa hajahamia upande wa pili, iliwapa shida Sana CCM kipindi hicho
Na baada ya maamzi ya Mh lowassa kutangaza kuhamia upinzani, wengi tuliamini huo ndio ulikuwa mwisho wa ccm, CCM washukuru kwamba waliyekuwa wamempitisha kuwa ndio mpeperusha bendera ya Uraisi, alibebwa na sifa zake binafs na sifa zake hizo ndizo zilizoibeba Ccm badala ya CCM kumbeba Magufuli, JPM ndio aliibeba CCM, na ndio maana hata Kampeni zake ilikuwa ( Chagua Magufuli) na si chagua CCM
Maana yake Huyu JpM alijibeba mwenyewe,
Nikurudishe kwenye hoja yako unayomshambulia JPm kwamba, eti alivyovifanya Vyote vilikuwa ni maono ya Jk, wewe unachokisahau ni kimoja tu na sina hakika unakisahau au tu Kwa sababu ya uharaka wa kuona makosa bila kujiuliza ni Nani anastahili kubebeshwa laumu hizo (makosa hayo)
Chama huandaa Ilani ya miaka mitano mitano, na nilazima Wakati wanaandaa Ilani hizo wajiridhishe kwamba zitatekerezwa zote Kwa kipindi hicho cha miaka mitano!!!
Sjui unanielewa, baada ya Ilani hizo kukamilika, hupew la anayewania nafasi ya Rais ili kunadi Sera hizo akiwa na uhakika atazifanya, sasa ikitokea hakuna utekerezaji wa Ilani hiyo, ama utekerezaji umekuwa busu, bado mambo hayo yaliyoahidiwa yatabaki kuwa deni Kwa Chama na si Kwa aliyekuwa Raisi,. Ni lazima ahadi hizo zitekerezwe Kwa awamu itakayofuata, na ndicho alichokifanya Mh JPM, alipewa viporo vilivyowashinda awamu iliyopita na mambo mapya mengine ya kutekerezwa
Sasa unapokuja kumlaumu Magufuli eti kwamba hajafanya zaidi Sana kafanya mambo ya kikwete ni kumwonea, Abayetakiwa kulaumiwa ni huyo Kikwete kwamba, Kwa nini hakuyafanya ktk vipindi vyake ikiwa Ilani ya uchaguzi huwa na vitu fanywa vya miaka mitanomitano??
Licha ya kufanya viporo lakini pia karibu asilimia zote kafanya yote aliyokuwa akiyanadi kuwa atayafanya, na ameenda mbali zaidi kufanya hata Yale ambayo hayakuwa kwenye Ilani ya CCM, utamlaumje huyu mtu
Kwenye swala la ujenzi na usimamizi, wa fedha, kivyovyote Mimi Magufuli namweka kuwa ndiye Raisi pekee Tanzania aliyeweza kusimamia vizuri kuliko maraisi wote Tanzania Kwa sasa
Swala la Nani atashindana naye ktk uchaguzi mwaka huu, Kwa kifupi na Kwa haraka Sana, atakayepatikana Kutokea upinzani yeyote Yule, hamuupendi ukweli, sasa nakwambia na nasisitiza kwamba, Watashindana lakini hawatashinda, shikilia Hilo mkuu, wembe ni uleule uliombeba JpM Kwa uchapa kazi wake ndio huo tena utambeba, Asante