Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577


Leo chama chetu kinampokea rasmi Ndugu Benard Membe ndani ya chama.

Kiongozi wa chama, Ndugu Zitto Kabwe; Mwenyekiti wa Chama Taifa, Ndugu Maalim Seif Sharifu Hamadi; na Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu Ado Shaibu na viongozi wengine wa chama wa Bara na Zanzibar wote watawaongoza wanachama kumpokea Ndugu Membe.

Karibu Benard Membe ACT–Wazalendo.

-----------UPDATE-----------

HOTUBA ALIYOITOA WAKATI WA KUKARIBISWA KATIKA CHAMA CHA ACT WAZALENDO SIKU YA TAREHE 16TH JULY 2020 MLIMANI CITY HALL


Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe- Kiongozi Mkuu wa Chama ACT Wazalendo.

Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hammad- Mwenyekiti wa ACT Wazalendo.

Mheshimiwa Ado Shaibu- Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo.

Viongozi mbalimbali wa Chama cha ACT wa ngazi zote, Wageni waalikwa,

Wawanachama wenzangu,

Mabibi na mabwana: Asalaam Alikuum Bwana yesu asifiwe. Awali ya yote,

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa wa Rehema, Mwenye kutupa uzima na kutuwezesha kuvumilia majaribu, kwani bila yeye hakuna kinachowezekana:

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa viongozi wa ACT Wazalendo kwa kunikaribisha kwa mikono miwili. Najisikia nipo salama, nipo huru, na najisikia nipo nyumbani. Ahsanteni sana na Mungu awabariki.

Kwa hiari yangu mwenyewe nimejiunga katika familia kubwa ya kupigania haki, demokrasia na mabadiliko yenye lengo la kuwanufaisha walio wengi ambao ni wakulima, wafanya biashara, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji ambao na pia wenye biashara zao halali.



Kwanini ACT Wazalendo?

Nina sababu chache kwanini nimeamua kujiunga na chama hiki ili kufanya kazi na viongozi na wanachama wake katika kushawishi wananchi wa Tanzania

Kuleta Madadiliko Nchini.

1. ACT Wazalendo ni chama kinachokua kwa kasi zaidi hapa nchini. Nimesoma katiba ya chama hiki na kuridhika kuwa ni jukwaa sahihi kwangu kutoa mchango wangu kwa nchi yangu.Imani kubwa ya chama hiki katika Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi, Msimamo wake kuhusu Muungano wa Tanzania wenye Usawa, haki na kuheshimiana na shabaha yake ya kujenga Tanzania na Zanzibar zenye Uchumi Shirikishi na jumuifu ni baadhi tu ya mambo yaliyonivutia kujiunga na ACT

2. Mimi nimefukuzwa CCM kutokana na Msimamo wangu wa kukosoa Serikali na kuonyesha nia ya kutaka kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi. Aidha kwenye ACT Wazalendo kuna viongozi ambao walipitia niliyopitia mimi.Kilichonivutia sio kufukuzwa kwao bali ni kutokata tama kwao. Maalim Seif Sharif Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe wanatupa funzo moja kubwa watanzania kuwa kutokata tama ni silaha muhimu sana kwa kila mwanasiasa makini na mwenye shabaha ya kweli ya kutetea Demokrasia. Nimejiunga na ACT Wazalendo kwa sababu viongozi wake na wananchama wake wengi ni watu majasiri wasiokata tama hata kama wanakutana na vikwazo visivyovumilika.

3. Tangu mwaka 2016 nchi yetu imekutwa na mitihani mingi kiungozi. ACT wazalendo ni chama ambacho kimesimama kidete kupaza sauti bila kuchoka na bila kujali itikadi ya mtu anayeonewa.Uchaguzi wa Zanzibar ulipofutwa, ACT Wazalendo walisimama na Wazanzibari. Ben Saanane alipotekwa ACT Wazalendo walisimama na CHADEMA, Diwani wa CCM Kanguye alipotekwa ACT Wazalendo walisimama na watu wa Kibondo. Wavuvi walipochomewa nyavu zao ACT Wazalendo walisimama nao. Wakulima wa Korosho walipoonewa ACT Wazalendo walisimama nao. Wafanyabiashara walipofungwa jela ACT Wazalendo ilisimama nao. Waandishi wa Habari walipotekwa au kufungwa kwa makosa ya kubambikizwa ACT Wazalendo ilipaza sauti. Hakika kila aliyeonewa, kukandamizwa na kunyanyaswa ilisikika sauti ya ACT Wazalendo ikimtetea bila kujali Chama chake.Sikuwa na namna nyingine isipokuwa kujiunga na ACT Wazalendo ili nami sio tu nipaze sauti bali pia nisaidiane na viongozi na Wanachama wa ACT Wazalendo katika kuhami Demokrasia na kuirejesha Tanzania kwenye mstari wa Haki.

Nimesema leo nina furaha kubwa ya kutambulishwa rasmi kama Mwananchama wa chama hiki. Ninawaahidi wananchama wote kuwa sitawaangusha na kuwa pamoja nanyi katika kila hali. Ninajua Watanzania wana mashaka makubwa na sisi tuliotoka CCM.Ninataka kuwahakikishia kuwa nina mwomba Mungu kila wakati ili niweze kutimiza dhamira yangu ya kuwa nanyi mpaka mwisho wa safari yetu. Maneno yangu yanaweza kuonekana matupu lakini vitendo vyangu vitaonyesha uhalisia.Tutaonyesha watu wanavyodhani sivyo(we will prove them wrong). Nina mzigo mkubwa wa kuonyesha hilo kwa Umma. Mungu atatusaidia kuonyesha hilo.

Kwa mazingira ya Tanzania na jukumu lililo mbele yetu hatuna budi kujenga ushirikiano mpana wa vyama vya siasa katika kukabiliana na chama tawala. Nitatumia uzoefu wangu kama Waziri wa mambo ya Nje wa muda mrefu katika kujenga mahusiano ya ushirikiano wa vyama. Hatupaswi kugawanywa na maslahi yetu binafsi kwani wajibu uliopo mbele yetu ni mkubwa sana. Tofauti zetu ni ndogo kulinganisha na maslahi mapana ya Tanzania yenye maendeleo, Demokrasia, Uhuru, na furaha.

ACT Wazalendo tukiingia Ikulu October 2020.

1. Tutashughulikia kwa ukamilifu tatizo la ajira kwa vijana na wale wahitimu wa vyuo vikuu ambao wapo vijiweni bila kazi.

2. Suala la mishahara ya watumishi wa vyombo vya usalama litapata kipaumbele.

Tutapandisha mishahara ya wafanyakazi wote ambao kwa kipindi chote cha miaka mitano hawajapata nyongeza za mishahara na promotion.

3.Kwenye utawala wetu tutapanua wigo wa demokrasia, Uhuru na kuheshimu haki za binadamu.

Hamtasikia tena kuwa kuna udukuzi au watu wasiojulikana.

Hukutakuwa na hofu ya kutekwa, kutumbuliwa wala hofu ya kupoteza uhai kwenye utawala wetu.

4. Tutajenga mazingira mazuri tena kwa ajili ya kuvutia wawekezaji. 5. Tutaimarisha sekta ya kilimo.

6. Tutaimarisha sekta binafsi iwe kweli engine ya maendeleo ya uchumi wetu.

7. Tutaimarisha Economic Diplomacy na kurejesha mahusiano ya kimataifa ambayo yameathirika vibaya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

8. Tutawaheshimu, tutawatendea haki na tutawapa moyo wafanyabiashara na ikiwezekana kuwarudisha wote walioihama nchi.Wafanyabiashara siyo maadui wa Serekali bali ni marafiki.

9. Serikali yetu itaheshimu utawala wa sheria, na itaanzisha tena mchakato wa katiba mpya.

10. Bei za mazao ya Pamba, Korosho, Ufuta, Alizeti, Mbaazi zitatafutiwa masoko ya kuaminika ili wakulima wapate kuuza mazao yao.

11. Bagamoyo Port expansion itapewa kipaumbele.

12. Mradi wa Gasi ya Lindi/Mtwara- Utapata kipaumbele.

13.Bureu du Change zote tutazirudisha na madai yote halali ya wafanyabiashara wa maduka ya kubadilisha fedha yatashughulikiwa na kulipwa.

Mwisho niwaombe;

Wananchi wote wawe wana CCM, wanachama wa vyama vya upinzani na watanzania ambao hawana vyama lakini wana haki ya kupiga kura karibuni ACT- Wazalendo Wale wote mlioniambia ulipo tupo, njooni kwa wingi kwa mamia na kwa maelfu ACT Wazalendo. Tunataka Kuchukua Nchi Mwaka Huu.

Ahsanteni sana Wana ACT- Wazalendo kwa kunikaribisha. Subirini maelfu ya watu watakaojiunga na ACT Kuanzia leo hii. Naomba Muwakaribishe kama mlivyonikaribisha mimi.

Zaidi, soma:

Uchaguzi 2020 - Bernard Membe achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Picha kutoka eneo la tukio
1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg

6.jpg
 
ACT Wazalendo,

Hivi CCM yangu nao hawana Verified Account yao hapa Jamvini JamiiForums? Kama hawana 'wananiangusha' mno na ninaomba wawe nayo pia.

Ujanja wote wa chama chako cha CCM ni kule mtaani tu kwa Watanzania "Wanyonge". Kwenye mitandao mfano humu Jamii Forums, wanaogopa bila shaka kutokana na madudu yao wanayotufanyia Watanzania.

Zaidi tu wanawakilishwa na wadau wao kama wewe mwenyewe, jingalao, Bia yetu, mr chopa, kuku mweupe, Kawe Alumni, Etwege, Magonjwa Mtambuka, na mwanachama mwenzenu mpya kabisa Pascal Mayalla.
 
Hiki chama chenu hata hakieleweki, hivi kati ya Mwenyekiti wa chama na Kiongozi wa chama ni nani mwenye nguvu ndani ya chama! Nani anampagia mwenzie majukumu? Na Membe atakuwa na cheo gn? Dah kizunguzungu tu
Huo ni mfumo wao tu. Israel na India zina marais na Waziri mkuu. Lakini PM ana nguvu kuliko Rais wakati Bongo Rais ana nguvu kuliko PM!
 
Yaah tunajua in long run upinzani unajengwa in ACT

Sema Tz ujasusi wa kishamba sana aisee
 
Kumfananisha Membe na Lowasa/Sumaye/Nyalandu si sawa, Membe mfananishe na Maalim Seif maana wamefukuzwa uanachama ndani ya CCM kutokana na misimamo yao.

Narudia tena, tofauti ya Lowassa na Membe, mmoja anapaka nywele picko, na mwingine kaachia mvi zionekane. Membe hakufukuzwa ccm, bali aligoma kuomba msamaha, kisha akazira na kurudisha kadi ya ccm. Katika mazingira hayo akaiacha ccm bila uchaguzi zaidi ya wao kuhitimisha kwa kutangaza kumfukuza.
 
Back
Top Bottom