GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kuna mmoja alisema ccm sio baba yake wala mama yake leo analamba miguu ya jiwe
Maalimu Seif alifukuzwa kwa tuhuma za kuutaka uraisi wa Zanzibar na msimamo wake wa Serikali tatu. Utakuwa umezaliwa juzi na wala hufuatilii dulu za kisiasa za nchi hii au wewe Mnywaranda.
Hautaki mjinga halafu ndo anakutawala sasa nani mjinga hapo..😂😂Hatutaki wajinga humu jamvini
Ila kweli hata mbunge mmoja wanaweza wasimpate kama Zitto hagombei,hata akigombea naona wazi uchaguzi huu CCM watatumia mabavu kupora majimbo yote
Agustino Lyatongo MremaKuna mmoja alisema ccm sio baba yake wala mama yake leo analamba miguu ya jiwe
Na hata Ukimchunguza ' Kiumakini ' kabisa huyu Mtu Mkuu utagundua ya kuwa ana ' CV ' Kali ya Serikalini, Foreign na hata alipokuwa Idarani pia.
Umeanza vizuri sana Maelezo yako na nikaanza Kukuona ni ' Mwerevu ' ila ulivyomalizia hapo mwishoni nimegundua una ' Upopoma ' mwingi tu!!!
Lowassa alijitoa CCM kwenda kujaribu bahati ya urais. Kilichompeleka upinzani ni TAMAAM YA URAIS.
Membe AMEFUKUZWA CCM sababu ya kudai haki za kikatiba. Kinachompeleka upinzani SIO URAIS bali ni kutafuta HAKI.
Kachero ni Kachero tuu.
Rudi usome tena nilichoandika. Membe hajafukuzwa kwa msimamo wa kiharakati, ni kwasababu ya tamaa na kujiona ana wanachama wengi nyuma yake, hauwezi kulinganisha na sababu zilizomfukuzisha Maalim
duuuh . . . . .Ujasusi Sebuleni Kwetu
Unaandika utopolo tu,wasiokuwa na msimamo wote wameomba msamaha. Kuutaka uraisi kwa njia ya kidemokrasia ni uroho wa madaraka? Basi hata huyo Yesu wa Lugola ni mroho wa madaraka ndiyo maana alichapisha form moja tu.
Acha kukariri wewe Banyamulenge.
Nilipokuwa nasoma shule ya bweni A level, kuna jamaa alikuwa akilazimisha sana awekwe kwenye timu ya shule kwenda UMISETA.
Hiyo ni kwasababu alijiona ni maarufu kwa jina lake na alipenda sana kusifiwa.
Alifikia kufanya shopping ya vifaa vya michezo na akawa amejiandaa kwelikweli.
Alilobby huku na kule kwa mwalimu wa michezo na walimu wengine wakawa wanamuonyesha wanamuonea huruma, lakini kumbe walikuwa wakimwangalia tu akihangaika.
Jamaa alikuwa na tabia ya kukosa maadili ikiwemo tabia ya kutoroka kwenda vijijini kupata ulabu.
Lakini siku wachezaji wote wanapanda basi la kwenda kwenye UMISETA yalipotajwa majina yote kwenye orodha jina la jamaa halikutajwa na akawa "very disappointed".
Michezo ya UMISETA ilipokwisha alijikuta anakubali ukweli kwamba hakustahili kwenda huko.
Nimeishasema humu mara nyingi kwamba kiufundi na kimfumo haiwezekani kwa Bernard Membe kuwa raisi wa nchi hii.
Na hali hiyo inazidi kujidhihirisha.
Lissu na Membe wote hawatokuja wawe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Yaani na Wewe unaamini na unaaminishwa kabisa eti kuwa Bernard Membe ana Sifa kabisa za kuja kuwa Rais wa JMT Mkuu? Nimeshakudharau!
Sawa mzee, basi Membe anatufaa sana
Halafu Jamaa mwili wake unakibaridi utadhani ni mtu anayesimamia samaki na kutoa samaki kwenye majokofu pale bandarini Kwa ajiri ya kuwauzia wateja wa madale, kumbe ni jasusi wa ACT
Kwa vyovyote vile naona hesabu haziko upande wa Membe
Kuna swali nimekua najiuliza toka hizi harakati zake za kwenda ACT zianze. Hivi kwanini hakuondoka 2015 na Lowassa aje aimarishe huo upinzani halaf Lowassa agombee uRais
Mbona aliacha miaka 5 yote mpinzani wake ajisimike vizuri chama/dola??
Majibu ni mawili tu 1:Hana nia ya dhati na 2:Sio strategist mzuri
Na majibu yote hayo manaake ni moja tu. Hafai