Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Usinilishe maneno, hakuna mahali nilipotumia neno HAKUTEGEMEA. Najua Kiswahili vizuri sana, na halina synonym kwenye maneno niliyoyatumia kwenye post yangu.
 
Nani asiyejua mkataba wa wachina wa Bandari ya Bagamoyo ni kuuza nchi kwa wachina na kutawaliwa kimawasiliano? Nani asiyejua ni mkataba wa kukubaliwa na wehu?

Anataka kuuza nchi kwa wachina huyu msaliti wa nchi nzima, alitaka urais mwaka huu kinyume cha muongozo wa CCM lakini akashindwa, sasa akakimbilia ACT Wazalendo ili agombee urais kujinufaisha yeye na wachina.

Lakini Zitto tayari anagombea, anafikiri atapewa kipaumbele kama Lowassa, hapo anatamani wapinzani wote wachague mgombea mmoja na awe yeye.

Hana lolote ila kuturudisha nyuma kwenye ukombozi wa nchi na kutugawanya, uanachama wake ACT Wazalendo ni wa uongo, akishindwa urais atarudi CCM iliyomsamehe.

===


Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mwanasiasa na Mwanadiplomasia mkongwe Bernard Membe amesema kuwa serikali ya Chama cha ACT-Wazalendo itakapoingia madarakani Oktoba 2020 itarejesha mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na mradi wa gesi wa Mtwara kwa sababu itatoa ajira nyingi kwa wananchi na kusaidia kukua kwa uchumi kunakogusa maisha ya Watanzania moja kwa moja.
 
Mbona hata sasa ipo hivyo hivyo? Uliza kina Mwigulu, Simbachawene etc.
Mkuu mbona nimeshasema kwenye hiyo post au haujasoma vizuri? Tena nimemtaja Mwigulu.
Tulia usome taratibu kiongozi wangu.
 
I am not sure who is fooling who here but I am almost certain Zitto is fooling Membe big time (and all ACT members for that matter...)
 
Najaribu kufikiria, kama vipaumbele vyake ndivyo hivyo alivyoainisha, atakuwa msaada kwa ACT au ndio atawadidimiza!
Upinzan unakwenda kugawanyika wenyewe kwa wenyewe, huu ni uchochoro kwa yesu bongo
 
Hicho kipaumbele Cha HAKUNA HOFU YA KUTUMBUANA KINATURUDISHA NYUMA! UFISADI WA WAZIWAZI!
Membe ataturudisha nyuma kubebana
 
Suala la mishahara ya vyombo vya usalama litapewa kipaumbele...mzee Membe unamaanisha nini?
 
Michezo vipi? Mtawezesha ujenzi wa viwanja vy Kisasa walau vya kuingia watu 20,000? au sio kipaumbele chenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…