Uchaguzi 2020 Bernard Membe is a real deal. Membe for president!

Tukiendelea kumvumilia aliyepo hali ya demokrasia yetu itakuwaje?, Ataiua kabisa, maana huyu anataka udikteta nchini

Bora tumchallenge tuwaache wananchi waamue kwani shida ni nini?
Demokrasi ni utawala mabao wananchi ndio wanaochagua viongozi wao; nchi zisizo na demokrasi ni zile ambazo wananchi hawana uhuru wa kuchagua viongozi wao- ama kuna uchaguzi ambao serikali inahakikisha kuwa inajua umepigia nani kura na itakushugulikia iwapo hutapiga kura hiyo kwa mtalwa (kama ilivyokuwa Iraq wakati wa Saddam) au kuna kura halisi ya uongozi wa kati lakini uongozi wa juu hauchaguliwi (kama ilivyo Iran) au hakuna uchaguzi kabisa (kama ilivyo Korea ya kusini); je ni demokrasi gani inayokosekana Tanzania?

Kugombana na mtawala siyo kukosekana kwa demokrasia, kunaweza kuwa ni kukosekana kwa haki za binadamu, lakini siyo kukosekana kwa demokrasia. Linapokuja swala la haki za binadamu pia uweke bayana kuwa haki hizo hazitumiki kuvunja sheria. Haki zote za binadamu zinataka mambo mawili makubwa yafuatwe: (a) haki hizo zisitumike kuvunja sheria za nchi, na vile vile (c) zisitumike kuathiri haki za binadamu wengine. Yaani huwezi kusema una uhuru wa kwenda na kuishi popote ukaamua kwenda kuishi Ikulu, utakuwa umevunja sheria. Lakini vile vile huwezi kusema una haki ya kufanya lolote, ukaamua kumuua mtu mwingine, utakuwa siyo tu umevunja sheria lakini vile vile utakuwa umeingilia haki ya kuishi ya victim wako; kwa yote hayo utaadhibiwa.

Kumekuwa na nyimbo sana za "kuminya demokrasi" bila kujua maana ya demokrasi ni nini; haina maana unayodhani. Hata kama rais ni mkrorfi, bado ni nchi ya kidemokrasi.
 
Kuna vingine na vyq maana na kuna vingine vya kipuuzi yani mm huu ni mwezi wa 9 cna job sasa magufuli anahusiana vipi come on every man to succeed is by his effort. Tafadhali usituwekee points za tangia lapili hadi chuo walk the talk. Say exactly what is reality.
 

Kuzuia vyama vya siasa kufanya siasa kinyume cha katiba na sheria, kutunga sheria za kuwapa baadhi ya watu impunity wasishtakiwe, kufungiafungia magazeti yenye mrengo tofauti wa kisiasa, kukamatakamata na kutia ndani wapinzani wako wa kisiasa mara kwa mara kwa sababu za kisiasa, Kuvuruga chaguzi za serikali za mitaa na kujipa ushindi wa 98%, kila kykicha kuwapelekea wapinzani askari ili wasifanye hata mikutano ya ndani BILA SHAKA MATENDO HAYO siyo Demokrasia.

Demokrasia siyo uchaguzi peke yake, Demokrasia ni suala pana na ni suala mtambuka, Demokrasia ni mchakato siyo tukio moja la uchaguzi.

Hata huo uchaguzi unaousema, bongo siku hizi uchaguzi hauheshimiwi, majuzi hapa kwenye chaguzi za serikali za mitaa kuna mambo ya ajabu kabisa serikali hii imefanya kufrustrate mchakato, ni. mambo ya ajabuajabu!

Mzee, Obama aliwaeleza viongozi wa Afrika, demokrasia siyo uchaguzi pekee, uchaguzi ni sehemu ya mchakato tu!
 
Yote uliyoorodhesha hapo yanaathiri demokrasi lakini zote hizo ni speculations tu, uchaguzi wa mitaa baadhi ya vyama havikushiriki kwa sababu zao wenyewe. Mwaka 1958 TANU ilitaka kukaa kushiriki uchaguzi wa kura tatu Nyerere akawaambia kuwa kutoshiriki ni kukubali kushindwa.

Mengine yote ni speculations na misrepresentations tu; nitaongea hili la kufungia magazeti. Ni kweli kuwa kufungia magazeti ni kosa, ila siyo kosa la serikali bali ni kosa la sheria inayotumika kuyafungia. Sheria hiyo ina walakini sana, lakini kwa vile ndiyo sheria iliyopitishwa na bunge ambayo inapaswa kuheshimwa. Utaratibu siyo kuikiuka bali na kuweka pressure ibadilishwe. Kama spidi limiti kwenye highway ni 30kph, lakini barabara yenyewe iko porini ambapo hakuna hata wapita njia, huwezi kuendesha 100kph ukidai kuwa spidi limiti ya 30kph ni ya hovyo. Ukishikwa utaadhibiwa tu.
 

Naona unajicontradict tu.

Sheria ya Magzeti ya leo imetungwa na serikali hii hii, yenyewe ndiyo iliyopeleka muswada bungeni Nape Nnauye wakati huo akiwa waziri wa habari, na ikasainiwa na rais wa serikali hiihii, kwa hiyo serikali hii iko complicit na ubanaji wa vyombo vya habari.

Nafurahi umekiri kuwa niliyoorodhesha yaanathiri demokrasia ila nakushangaa unapodai ni speculation hahahah, Mzee uko out of touch au una mahaba na Magufuli, kama huoni jinsi utawala wa Magufuli unavyoharass wapinzani na kuwanyima nafasi ya kufanya shughuli halali za kisiasa na kuwaswekasweka ndani basi pengine una upofu au una mahaba mazito na Magufuli.

Kama huoni kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 ni fair, huru na haki basi You are more than blind.

Pole sana mzee!
 
Hata APPT MAENDELEO ni chama cha upinzani, aende huko. Au intelijensia yake ni lazima agombee urais tu? Uza ubongo huo boss maana unakaa nao kwa hasara. Kosa la Lowassa hatuna muda wa kulirudia tena
Mkuu Tindo, kupanga ni kuchagua. Vyama vya upinzani siku zote vimenyimwa nafasi ya kuendesha shughuli zao halali za kisiasa kwa mujibu wa sheria hapa nchini. Na kwa kuzingatia uhuru na haki zote zilizoainishwa kikatiba havina nafasi ya kujijenga toka kipindi ilipoingia madarakani awamu hii ya tano.

Nafikiri tunahitaji mtu sahihi wa kuviunganisha vyama vya upinzani pamoja ili vikapate kudhamiria na kuaminika kuitwaa Dola toka mikononi mwa chama tawala. Licha ya mapungufu yaliyojitokeza wakati ule wa Lowassa, isiwe sababu ya kutouona umuhimu wa kujaribu kufanya hivyo kwa mara nyingine.
 
No wonder somebody invented examination. Examination sets level of understanding. When you think or believe to know, we prove you right or wrong by subjecting you to examination. There you get to know your literacy. What you have written is just a false wish, baseless and proves some sort of ignorance.

Look here. Can you vindicate this man from all the stupid things that happened during the last election? Can you hope to see Membe at a higher level of intelligence than his previous failing state? Membe needs a psychologist to help him realize where he belongs. In my life, I have met several people under such psychological trauma, such that they would wear a winter coat in the middle of tropical hot weather. Ask them why? like Membe, I will pick the form for the presidency, they will say it is cold here! Total misinterpretation of the truth!!
 

Una matatizo ndugu yangu; serikali haitungi sheria hata siku moja. Kazi ya serikali ni kusimamia sheria ambazo zinatungwa na Bunge tu; ndiyo maana linaitwa baraza la kutunga sheria. Kama Bunge lilipitisha, basi serikali itazisimamia. Usihangaike na aliyepeleka muswada, kwani hiyo ni proposal tu ambayo huweza kukataliwa na Bunge.

Sasa iwapo bunge lilipitisha basi inakuwa ni sheria, na kosa siyo la aliyepeleka proposal ile bali yule aliyepitisha iwe sheria. sahihi ya raisi ni ya uhitimishaji tu; asipohitisha, inabidi bunge livunjwe uitisweh uchaguzi mwingine, jambo ambalo ni costly ndiyo maana hakuna rais aliyewahi kukataa kusaini sheria iliyotungwa na bunge. Katiba mpya inatakiwa ili kurekebisha kipengele hicho, lakini bado tunaishi chini ya katiba iliyopo.
 
wewe hujachoshwa na utawala uliofeli wa Jiwe?, una moyo kweli wewe!
bora kubaki na huyu huyu kuliko wewe unayejidanganya kitu ambacho unajua rohoni kwako hakiwezi kutokea hata kama atapata ridhaa ya vyama vyote vya upinzani. Na nina wasiwasi kama kweli wewe ni mtu wa upinzani wa kweli sababu kama ungekua wa kweli ungejua kama huyu Maembe Mrema Lowasa na Sumaye hawakua na nia yoyote nzuri ya kuwaongoza ninyi bali ni uroho wa kuwa viongozi tu. Bora hata Nyalandu japo simuamini pia lakini anaweza kuwa na sababu siyo hawa wanaokatwa mikia halafu wanakimbilia kuomba huruma ya wananchi.
 


Unataka tukuamini kuwa gari limeharibika engine , unalitengeneza kwenye mwendo ??
 

Mkuu bado unaabudu sanamu? Kama umekula hela ya Membe mrudushie tafadhali. Yaani kweli kabisa unaamini mtu toka ccm ndio anaweza kuwaongoza wapinzani! Tafadhali sana mkuu nakuheshimu.
 
Membe siyo mtu sahihi
 
View attachment 1495154this is CCM siku moja mtapiga magoti kwa wananchi

Haswa watazame namna vyombo vya dora wanavyowafanya wapinzani sbb chuki inapikwa kwa ujinga wa hali ya juu inawezekana tukaumia wote siku hiyo ikifika. CCM wajitenge na vyombo vya dola na wapinzani waachiwe kufanya siasa haswa kipindi hichi.
 
Jirani ni balaa. I hate Membe but at the moment I hate Magufuli more than Membe. Wapinzani wakiweka tofauti zao pembeni wakaweka mgombea mmoja hata kama asipokuwa Membe. I tell you Magufuli atakuwa kwenye side mbaya sana.
Victoire Ukifanya Analyis ya ukweli Magu anapendwa sana, Dar kidogo kuna zile siasa za upinzani upinzani, lakini ukiondoa hilo hakuna unayeweza kumshindanisha naye, Fanya research mwenyewe. Kwa habari ya Membe? Hizo ni propaganda tu na weakness ya Wapinzani kudaka makapi ya CCM wakidhani wataleta changamoto ya kweli.
 
Ni kweli Magufuli anapendwa sana na wananchi. Tatizo wananchi wamezoea tabu. Mimi nilikuwa nasemea nafsi yangu.
 
Ni kweli Magufuli anapendwa sana na wananchi. Tatizo wananchi wamezoea tabu. Mimi nilikuwa nasemea nafsi yangu.
Hapana Mama wananchi hatujazoea taabu, Unafikiri wanasiasa wanaweza kutuondolea matatizo yetu? Hawawezi, ila kila Rais anapokuja kuna kundi linaloingia kufaidi na wengine wanapoteza, lakini tuliowengi tunaishi maisha yetu yale yale ya siku zote, siyo ya kuzoea taabu bali kwa nguvu zetu, kila pesa unapata kwa halali,bila wizi, bila rushwa.
Ukiondoa biashara ndogondogo lakini Capital investments zote zinafanyika kwa kipato halali, tena mshahara.
 

Magu hapendwi na wananchi kwa kiwango unachodhani, ila umeaminishwa kuwa anapendwa na wananchi sana kwa sababu
1. Mosi, sauti huru na mbadala za kusikika, na kupata maoni ya wananchi zimeminywa. Hata TWAWEZA iliyokuwa ikikusnya tafiti za wananchi ilipata msukosuko mkubwa kwa kuleta tafiti inayoonyesha kuporomoka umaarufu wa kutisha ea Bwana Mkubwa.

2. Kuna propaganda kali ya kumpa promo bwana mkubwa, hii ni kuanzia kwa vyombo vya serikali na vingine vilivyoanzishwa kwa lengo hilo, na vyombo vingine visivyokwenda na beats vinanyang'anywa leseni (mfano Tanzania Daima), kwa hiyo ni vigumu kupata uhalisia wa msimamo wa wananchi

3. Vyama vya siasa vimezuiwa kufanya siasa zake smoothly, vinasumbuliwa sana, hata mikutano ya ndani nayo wanakuwa harrassed, CCM ndo pekee inayopewa mazingira mazuri ya kufanya siasa, Sasa kwa sasa usidhani eti huu ukimya wa wananchi ni ishara ya Wananchi kumkubali Magufuli. No hii ni wrong assesment

4. Uchaguzi wa serikali za mitaa ungetoa picha ya kukubalika Magufuli, lakini kwa hofu ya CCM kushindwa na pia kuwapa momentum wapinzani akaamua kuuvuruga na kuipa CCM ushindi wa 98%.

Nakueleza hivi:

1. Subiri kampeni za uchaguzi zianze ndo utajua kuwa watu hawana mpango na wala hawababaishwi na propaganda mfu za CCM.

2. CCM wanajua wakiweka level ground za kisiasa nchini, wakawapa wapinzani haki yao ya kufanya siasa kwa mujibu wa katiba, CCM wanapoteza mara moja tu

3. Magufuli kaharibu maisha ya watu, kwenye utawala wake vyuma vimekaza kupita kiasi, kaumiza watu wengi, wafanyakazi kawaminya maslahi yao, biashara nyingi za watu zimekufa

Hitimisho ni kwamba usione wananchi wamekaa kimya, wanaugulia maumivu, hawana pa kusemea baada ya huyu bwana kwa hofu yake kuparalyse demokrasia nchini, Ngoja uchaguzi uje ndo utajua kuwa hakubaliki kwa kiwango usichokitarajia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…