Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Jasusi wa zamani wa TISS, Mwanadiplomasia na waziri mstaafu Benard Membe yupo kimya Sana awamu hii.
Membe ni jasiri aliyemtikisa Magufuli na kukosoa utendaji wake tangu mwaka 2016 mwanzoni. Namnukuu"Rais Magufuli asitudanganye eti kapunguza matumizi ya serikali kwa kuunganisha wizara mbalimbali, alichokifanya ni sawa na kupunguza mifuko huku idadi ya mayai ikiwa ileile, yaani kahamishia mayai ktk mifuko michache na sio kuyapunguza mayai. Kama anadai kapunguza wizara ngoja tuone bajeti yake ya Kwanza mwaka huu 2016". Benard Membe.
Alipotoa kauli hiyo alitukanwa Sana na UVCCM ya kipindi hicho. Baada ya hapo alinyamaza kimya na kuibuka baadae na kudai atampinga Rais Magufuli kwa njia ya uchaguzi ndani ya chama 2020. Hawakumvumilia na badala yake alifukuzwa na kuhamia ACT. Aligombea Urais na kuambulia kura chache mno, kura si zaidi ya 60,000.
Je, jasusi huyu yupo wapi mbona hasikiki? Anautazama vipi utawala huu?