Bernard Membe mbona yupo kimya sana?

Bernard Membe mbona yupo kimya sana?

waliompa kazi na kuijua job description yake hawana shida naye wanajua kazi aliyoifanya...
 
afya baba, afya ni mali!.....usiwaone hawa wakubwa wanabeba vimwana kama wanashindania makombe ya "kugegeda"! Covid imetufumbua macho baada ya wengi kushindwa kwenda kwenye kliniki zao huko Spain, India nk. Haki ya nani itumieni miili yenu vizuri maana kuna wakati utakuwa unatembea na toolbox lako(begi la vidonge).
 
Jasusi wa zamani wa TISS, Mwanadiplomasia na waziri mstaafu Benard Membe yupo kimya Sana awamu hii.

Membe ni jasiri aliyemtikisa Magufuli na kukosoa utendaji wake tangu mwaka 2016 mwanzoni. Namnukuu"Rais Magufuli asitudanganye eti kapunguza matumizi ya serikali kwa kuunganisha wizara mbalimbali, alichokifanya ni sawa na kupunguza mifuko huku idadi ya mayai ikiwa ileile, yaani kahamishia mayai ktk mifuko michache na sio kuyapunguza mayai. Kama anadai kapunguza wizara ngoja tuone bajeti yake ya Kwanza mwaka huu 2016". Benard Membe.

Alipotoa kauli hiyo alitukanwa Sana na UVCCM ya kipindi hicho. Baada ya hapo alinyamaza kimya na kuibuka baadae na kudai atampinga Rais Magufuli kwa njia ya uchaguzi ndani ya chama 2020. Hawakumvumilia na badala yake alifukuzwa na kuhamia ACT. Aligombea Urais na kuambulia kura chache mno, kura si zaidi ya 60,000.

Je, jasusi huyu yupo wapi mbona hasikiki? Anautazama vipi utawala huu?

Kazi imeshaimaliza.. Au unaamini Ugonjwa wa moyo ulimuua Baba mwendazake
 
Anasubiri bao la dakika 89.
Jasusi wa zamani wa TISS, Mwanadiplomasia na waziri mstaafu Benard Membe yupo kimya Sana awamu hii.

Membe ni jasiri aliyemtikisa Magufuli na kukosoa utendaji wake tangu mwaka 2016 mwanzoni. Namnukuu"Rais Magufuli asitudanganye eti kapunguza matumizi ya serikali kwa kuunganisha wizara mbalimbali, alichokifanya ni sawa na kupunguza mifuko huku idadi ya mayai ikiwa ileile, yaani kahamishia mayai ktk mifuko michache na sio kuyapunguza mayai. Kama anadai kapunguza wizara ngoja tuone bajeti yake ya Kwanza mwaka huu 2016". Benard Membe.

Alipotoa kauli hiyo alitukanwa Sana na UVCCM ya kipindi hicho. Baada ya hapo alinyamaza kimya na kuibuka baadae na kudai atampinga Rais Magufuli kwa njia ya uchaguzi ndani ya chama 2020. Hawakumvumilia na badala yake alifukuzwa na kuhamia ACT. Aligombea Urais na kuambulia kura chache mno, kura si zaidi ya 60,000.

Je, jasusi huyu yupo wapi mbona hasikiki? Anautazama vipi utawala huu?
 
Bernard yuko kimya sababu anasubiria hukunu ya CAS!
 
Back
Top Bottom