Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Mimi sio kachero, nimegombea kuchukua kiti cha urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Hapo kwenye idadi kubwa ya wabunge waliomfuata naomba niwajue kwa anayewajua tafadhari
 
Nimetoka kusikiliza mahojiano ya mgombea urais wa JMT kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo muda mfupi uliopita kwenye kituo cha DW. Mtangazaji katupa maswali ambayo nilikuwa nikitamani sana siku moja kusikia BM mwenyewe akiyatolea ufafanuzi licha ya kusikia juu juu tu.

Moja kati ya swali ambalo kaulizwa ni kuhusu yeye kuhusishwa sana na ukachero na yawezekana kabisa akawa amepandikizwa na chama tawala ili kuuwa nguvu ya upinzani kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Bernard Kamillius Membe ameweka wazi kabisa kuwa, yeye ameamua mwenyewe kugombea na kuwania nafasi ya urais wa JMT wala sio pandikizi kama fikra za baadhi ya watu zinavyodai. "Kama ni kutumwa, unadhani nitakuwa nimetumwa na nani? Kwa lengo lipi? Au kwa kupata cheo kipi, ambacho kufumba na kufumbua unaweza kujikuta umetumbuliwa?", amesema Membe.

Mbali na hayo yote, Ndugu Bernard Kamillius Membe amesema kitendo cha yeye kuja ACT-Wazalendo ni kwa sababu ya kuchoshwa na mambo yalivyokuwa yakifanyika upande wa pili na ndiyo maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya wabunge waliomfuata na wala hawakwenda kwenye vyama vingine.

Source: DW
Membe hana ubavu wa kukataa hela za magufuli. Amechoka kimaisha na ananunulika kwa bei yeyote. Sio lazima ahaidiwe cheo, anaweza pewa hela kwa ajili ya kuvuruga mchakato wa upinzani kuchukua nchi.

Ila walichokosea waliomtuma ni kuwa, mwaka huu wananchi hawaaangalii Membe au nini??? Wanaangalia mwenye uwezo na dhamira ya dhati ya kuangusha utawala dhalimu wa Ccm na magufuli na huyo si mwingine Ila ni Tundu Antiphas Lissu
 
Huku upinzani ataondoka bila kugeuka nyuma...
hatutaki umbuzi kwenye mambo ya msingi.
 
..ndiyo maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya wabunge waliomfuata na wala hawakwenda kwenye vyama vingine.

Source: DW
Membe anatakiwa kuamka kutoka usingizini. Hao wabunge wengi sana atakuwa aliwaona ndotoni.

Huyu mzee sasa hivi ukimsikiliza na hata kumuangalia, mentally hayupo vizuri.
 
Nimetoka kusikiliza mahojiano ya mgombea urais wa JMT kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo muda mfupi uliopita kwenye kituo cha DW. Mtangazaji katupa maswali ambayo nilikuwa nikitamani sana siku moja kusikia BM mwenyewe akiyatolea ufafanuzi licha ya kusikia juu juu tu.

Moja kati ya swali ambalo kaulizwa ni kuhusu yeye kuhusishwa sana na ukachero na yawezekana kabisa akawa amepandikizwa na chama tawala ili kuuwa nguvu ya upinzani kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Bernard Kamillius Membe ameweka wazi kabisa kuwa, yeye ameamua mwenyewe kugombea na kuwania nafasi ya urais wa JMT wala sio pandikizi kama fikra za baadhi ya watu zinavyodai. "Kama ni kutumwa, unadhani nitakuwa nimetumwa na nani? Kwa lengo lipi? Au kwa kupata cheo kipi, ambacho kufumba na kufumbua unaweza kujikuta umetumbuliwa?", amesema Membe.

Mbali na hayo yote, Ndugu Bernard Kamillius Membe amesema kitendo cha yeye kuja ACT-Wazalendo ni kwa sababu ya kuchoshwa na mambo yalivyokuwa yakifanyika upande wa pili na ndiyo maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya wabunge waliomfuata na wala hawakwenda kwenye vyama vingine.

Source: DW
Jana wakati anasema kuna viapo hawezi kuvivunja tupo tuliomuelewa zaidi
 
Back
Top Bottom