Bernard Membe same old story

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Nataka Sana kuamini Bernard Membe ana kitu 'interesting'anakuja nacho lakini nashindwa.

Nionavyo Mimi story ya Bernard Membe itaishia kule kule ilipoishia ya Lowasa na Mrema na wengine.

Nashindwa kabisa kumtazama Bernard Membe kama 'mtu mwenye master plan'
Ya kumtoa Magufuli au hata kuleta Tu demokrasia ya kweli achilia mbali plan ya kukamata madaraka.

Makosa ya Bernard Membe ndo makosa ya Lowasa ..ndo makosa ya Chadema na kina Mrema na wengine.

Kosa kuu kabisa ni kushindwa kutazama events kabla hazijatokea na kutumia nafasi yako ku shape hizo events ..na soon atajikuta victims wa events ambazo

Wengi tunaona na tunajua ni predictable sababu trends ya siasa za Tanzania inajulikana kabisa..tofauti na Mrema ambae kabla ya kujitoa CCM na kwenda gombea urais kulikuwa hakujawahi kuwepo uchaguzi wa vyama vingi wala jaribio la kuleta katiba mpya..

Membe na Lowasa na wengine wa sasa wote wanajua uchaguzi unavyoendeshwa nchini..na wote wanajua tume ya uchaguzi ilivyo..na wote walikuwa na nafasi ya Ku shape things for future wakati wa Bunge la katiba

Laiti kama kina Lowasa ,Membe ,Nape ,lipumba ,Tundu lissu wangeungana kipindi cha Bunge la katiba na kuhakikisha nchi inapata tume huru ya uchaguzi..leo tungekuwa labda na Rais Lowasa au tunazungumzia uwezekano wa Membe kuwa Rais uchaguzi huu..

Lakini kushindwa kuona future na kufikiri siku zote maslahi yao yako CCM na yako pamoja na maslahi ya dolla ndo leo mtu kama Membe anatia huruma hata kabla hajaweza kugombea. Lowassa anatia huruma..Nape anatia huruma.. Lipumba huyu ndo aliongoza kina Tundu Lissu kususa Bunge la katiba anatia huruma.

Ukweli wanasiasa wengi wanatia huruma na watazidi kutia huruma hasa siku Magufuli atakapotangazwa Rais wa Maisha...

If only wangekuwa smart enough to see the obvious...wengeweza shape the future
Ila Kwa sasa most likely watakuwa the next victims wa same old story
Ya kulalamika uchaguzi haukuwa huru na blabla nyingine.

Mpaka tutakapo pata wanasiasa wa kutazama miaka 100 mbele ..kila siku Hali itakuwa hivi hivi same old story
 
Kila mtu ni mbinafsi, ila Waafrika tumezidi. Yanayotokea ni kwa sababu ya ubinafsi wao, as a result what goes around comes around.
 
Namnukuu Membe akihojiwa na DW jana:

"nisipopata haki yangu ya kugombea ndani ya ccm ntaitafuta nje ya ccm"
"unaweza kupanda basi toka mtama kwenda dar lakini ukishushwa njiani unapanda hata bodaboda kufika unakokwenda" mwisho wa kunukuu.

Membe anaenda ACT au chadema!

Wafuasi wa upinzani jiandaeni kudeki barabara zigo hilo laja.
 
Membe anataka Kamati Kuu ya CCM imuombe msamaha kwa kutangaza kuwa amefukuzwa CCM wakati haina nguvu hizo kikatiba!

Yaani anataka Kamati Kuu yenye wajumbe hawa imuombe msamaha;
1)Rais wa Tanzania
2)Rais wa Zanzibar
3)Makamu wa Rais wa Tanzania
4)Makamu wa Mwenyekiti bara(Mzee Mangula)
5)Katibu Mkuu wa CCM
6) Waziri Mkuu wa Tanzania
7)Waziri Kiongozi Zanzibar
8)Maspika wa mabunge (Tanzania na Wawakilishi)
9)Waziri Mkuu mstaafu(Mzee Pinda)
10)Wenyeviti wa Jumuiya za CCM

8)etc

Tanzania kuna vituko!
 
Nyie mchekeeni tu bipolar disorder anaenda kuzamisha hii nchi, anyway mabadiliko halisi yataletwa na watanzania wenyewe wasiwategemee wanasiasa kabisaa.
 
Tatizo la Tanzania ukiweka mkakati wa kumtoa MTU FURANI madarakani kupitia uchaguzi lazima wakudedishe.
 
If only wangekuwa smart enough to see the obvious...wengeweza shape the future
Ila Kwa sasa most likely watakuwa the next victims wa same old story
Ya kulalamika uchaguzi haukuwa huru na blabla nyingine.
Mkuu The Big Boss, kwanza asante kwa hii mada, naunga mkono hoja.

Haya sasa, kama mambo yenyewe ndio haya tukiwaambia watu humu kuwa CCM itatawala milele, mnakasirika!.
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P
 
Nyie mchekeeni tu bipolar disorder anaenda kuzamisha hii nchi, anyway mabadiliko halisi yataletwa na watanzania wenyewe wasiwategemee wanasiasa kabisaa.
Bwashee kwa hiyo kina Lissu, Mbowe, Nyalandu, Zitto wanatughilibu tu kumbe!
 
Membe anataka Kamati Kuu ya CCM imuombe msamaha kwa kutangaza kuwa amefukuzwa CCM wakati haina nguvu hizo kikatiba!

Yaani anataka Kamati Kuu yenye wajumbe hawa imuombe msamaha;
1)Rais wa Tanzania..!
Kweli hiki kituko [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
CCM waoga tu wa demokrasia. Kama wanaamini wanapendwa waache kukamatakamata wapinzani waone mziki wake
 
Mkuu The Boss, nakupa kongole kwa hoja murua ambazo umezianisha. Lkn nafikiri ni lazima tuangalie mazingira ambayo matukio ya mabadiliko yanapotokea, hali kadhalika na usimamizi wake unavyokuwa.

Kipindi cha Mrema alikuwapo Mwl. Nyerere, ambaye aliweza kuzuia mabadiliko kwa hoja murua kabisa, na hata kuweza kumnadi barabara mgombea wa CCM aliyeteuliwa. Baada ya Mkapa lilikuja kundi la mtandao ambalo liliweza kufanikisha chaguo lao na hata kuweza kumpa JK hatamu za uongozi wa awamu ya nne.

Awamu ya tano imekuja kwa uongozi wa bahati nasibu. Hali ambayo ilitokana na wanamtandao kukosa mrithi wa JK na hatimaye kujikuta wote wakiikosa nafasi ya mmoja wao kumrithi mtu wao.

Ujio wa JPM ulikuwa kama embe dodo ambalo limeokotwa pasipo kutarajia. Hali ambayo imempelekea kuendesha siasa kwa hisia badala ya msingi ya chama. Sasa kinachokea kwake ni kuwa ametengeneza uadui na CCM Asilia na kuamua kuambatana na machotara wa siasa andamizi.

Mkuu, kwa vyovyote vile, tusijaribu kulinganisha jitihada na matokeo ya vita hivi vya kugombea madaraka kwa mazingira ya sasa ya kisiasa. Membe bado ni mtu muhimu ambaye anaweza kubalisha "rules of the game" za siasa za wakati huu hapa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…