Bernard Membe: Tanzania diplomasia imeshuka awamu hii. Tutatengwa na majirani wakiona hatufuati vigezo vya WHO kupambana na COVID19

Bernard Membe: Tanzania diplomasia imeshuka awamu hii. Tutatengwa na majirani wakiona hatufuati vigezo vya WHO kupambana na COVID19

Nimesikiliza dw mchana huu mzee wa diplomasia kafunguka duuu...

Sent using Jamii Forums mobile app

Mashabiki na Wakereketwa wa CCM ya Jiwe Naona radio zote za nje mtaziita za MABEBERU.
Hii jioni BBC wanasema Madreva 25 wa Tanzania wamepimwa na kukutwa Wana Covid-19 na WAMEZUIWA kuingia Kenya.
Kwa hiyo BBC ni MABEBERU na Kenya wanatumiwa na Mabeberu....Nonsense!
 
Jidanganye kuna Beira Msumbiji na Welvisbay Namibia

Unajua Mafisccm wengi wanaongozwa na Ushabiki wa kijinga na wala hawajui hata Jiografia ya Africa& Dunia yote.
Mtu kufikiri eti Zambia ikifunga mpaka na Tanzania itakosa Bandari ya kupitisha bldhaa zake ni upuuzi mtupu!
 
Unajua Mafisccm wengi wanaongozwa na Ushabiki wa kijinga na wala hawajui hata Jiografia ya Africa& Dunia yote.
Mtu kufikiri eti Zambia ikifunga mpaka na Tanzania itakosa Bandari ya kupitisha bldhaa zake ni upuuzi mtupu!
Tena hili tukio la corona kupuuzwa na magufuli ndio wake up call yao

Ninavyowajua waZambia watabadili port sema waKongo ndio wataumia kidogo halafu na wao watahamia Namibia
 
Akihojiwa na DW, waziri wa zamani wa mambo ya nje mheshimiwa Bernard Camilius Membe amesema katika awamu hii ya utawala wa Magufuli, diplomasia imeshuka mno.

Membe anaonya kwamba, tanzania awamu hii inajiendeshea mambo kivyakevyake nje ya utaratibu wa jumuia ya kimataifa.

Akoingelea suala la korona, Membe amedai kuwa Tanzania haiheshimu na imejitenga na miiko ya shirika la afya WHO.

Chanzo: DW
=====


Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amezungumzia uhusiano wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na nchi za jirani katika kipindi hiki cha mlipuko wa #COVID19

Amesema kwasasa nchi zipo katika mapambanao dhidi ya #CoronaVirus na dio maana nchi kama Zambia zinafunga mipaka yake na kuzuia watu waziende ikiwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo kutoka sehemu moja

Amesema "Kama Zambia wamefunga mpaka wake na kuzuia magari yasipite, huo ni mkakati na hatua ya kuzuia maambukizi ya #COVID19 na ndio maana inatakiwa tufanye mambo haya kwa pamoja kwa pande zote mbili"

Aidha, kuhusu kupimwa kwa Madereva wa Tanzania wanaotaka kuingia Kenya, amesema kidiplomasia ni kwamba nchi za jirani zina wasiwasi sana kwamba Tanzania inaweza kuwa inapeleka ugonjwa huu kwenye nchi fulani

Ameeleza "Wasiwasi huu unaweza kuwa unakuja baada ya kuona pengine hatufungamani ni vigezo vya WHO ambavyo vimewekwa na dunia nzima vinavifuata labda mpaka pale tutakapofungamana na vigezo vya WHO wanavyofuata wenzetu"

Ameongeza "Kwa na mna Tanzania inavyoshungulikia jnaga kama hili tutatengwa, majirani watatutenga na kutengwa ni kwa namna hii ya kufunga mipaka na kidiplomasia tunasema mtengano huu unatumiiza na kututesa zaidi sisi kuliko majirani"

Amemalizia kuwa ni kweli diplomasia imeshuka kwasababu awamu hii haijengi kwenda na dunia inaangalia zaidi matatizo ya ndani na ina athari zake hasa tukipata janga hili na ndio maana tunasema diplomasia imeshuka sana
Membe amesahau wakati wake ambapo Tanzania ilikuwa imetengwa na Kenya na Uganda kwenye maamuzi hasa kwenye ujenzi wa treni za "standard gauge". Alipokuja Magufuli kila kitu kilibadilika. Bomba la Mafuta likapita kwetu. Standard gauge inajengwa kuunga nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Congo. Ile ya kuotokea Kenya kwenda Uganda imekufa. Sasa utasemaje diplomasia imekufa. Je wewe ulishindwa nini kutetea haya. Ulitengwa na mikutano ulikuwa huendi. Sasa hapa mwenye kushindwa kidiplomasia ni wewe au marehemu Mahiga! Ulitumia diplomasia kupata pesa ya kujenga kiwanda cha simenti kwetu, lakini ukaziweka zote mfukoni! Unataka uraisi ili ukope na kuweka mfukoni.
 
Back
Top Bottom