Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Bernard Morrisson BM3, the gifted one, King of Football ni mchezaji mwenye kasi/pace/speed na jitihada ya dhati ambayo Yanga ilikuwa inaikosa kwa muda mrefu,Benard Morrisson anajua kucheza kikubwa na kimalengo,hii ndiyo inayotakiwa katika hizi klabu kubwa hapa nchini, sina shaka na Simba ambayo ina wachezaji kama Jean Baleke na Moses Phiri,washambuliaji katili kwenye kumi na nane ukimkata atainuka na atafunga goli, Bernard Morrison ni aina ya mchezaji hao mfano wa Demba Ba,Christian Benteke,Roger Milla, Abedi Pele,Sulle Muntali na Samuel Etoo ambao walikuwa mastriker hatari na katili wa kiafrika kwenye kumi na nane ya timu pinzani,hii ndio hali na mori ya ushindi katika mpira wa kisasa unaochezwa duniani hasa tunapoanza na nyimbo yetu ile "Leooh leo ndio leo,Leooh kivumbi na Jasho"
Ufundi mwingi wa Bernard Morrisson unaweza kuibeba Yanga ambayo inacheza mpira wa pasi ambao inawapasa wachezaji wawe wenye uwezo wa kukimbia uwanjani pindi wawapo na mpira na pale wasipokuwa na mpira, Timu za waarabu hazina mafundi wengi wa soka ila wanajivunia uwezo wao wa kucheza mpira wa kasi,Yanga inacheza mpira wenye ufundi mwingi,inasukuma mpira taratibu kana kwamba wao ndio wanaongoza katika matokeo hata kama bado hawajashinda,wanaridhika sababu ya pira biliani wanalocheza lakini Yanga inahitaji kuwa na washambuliaji katili ambao wataweza kuweka mpira kambani huku wachezaji wengine wakiendelea na ball technic boli fleva huku wachezaji wengine wakicheza tu kimkakati na kasi ya uchezaji inayonufaisha kuweza kuondoka na ushindi. Yanga isiache mchezaji pinzani awazidi mbio na kufanikiwa kwenda kuonana na Kipa Djigue Diara uso kwa uso,Silaha kubwa ni mbio na munkari ya ushindi sio kwenda uwanjani kufanya jog tu .Wachezaji angalau wanampira wa kasi ni Tuisila Kisinda,Mudathir Yahya,Kennedy Musonda kwa upande wa Simba sina shaka ninapomuona Baleke aliyekuja sawa na Musonda akiwa na goli tisa.
Bernard Morrisson kama alivyo Kylian Mbape ni mchezaji mwenye mbio nyingi na ndio mafanikio yake yapo hapo anaisaidia timu,akishavuka miaka 30 ataendelea na kasi yake,rejea Ronaldo hajapotea akiwa na miaka 30, sasa hivi ana miaka 38 na msimu uliopita tu alikuwa anagombania ufungaji bora, mchezaji akifika miaka 38 ni mkubwa sana,malegend wengi wanastaafu chini ya miaka 35 huu ni ufundi mwingi,hali,mori,munkari na jitihada ya mchezaji kutokata tamaa hadi anapoona mpira upo kambani,kivumbi na jasho,hii ndio siri ya mawinga washambuliaji, hahitaji hata kufika miaka 30 kuweka legacy na stats za kutisha sana,kama Rooney, Owen, Neymar na golden boy wengine huwa wanastaafu mapema sababu wameanza kucheza at top level wakiwa wadogo,siri ni kasi,pace,mori ya ushindi nakosa neno zuri la kiswahili,munkari na jitihada za kuhakikisha unauingiza kambani mpira wowote unaokutana nao kwenye kumi na nane ya timu pinzani.
Nimalizie kwa kumpa tano ndugu Bernard Morrison,toto tundu mwenye uwezo kwenye kila kitu ball balance,ball skills and ball brain. Bernard Morrisson ata akikaa miaka miwili bila ya kutrain akiingia uwanjan bado ataweza kufanya maajabu tofauti na wachezaji wengine manguvu kibao wakifika 30+ wanakuwa maflop,Ushauri wangu kwa Bernard Morrison,kikubwa tu ni nidhamu ya soka lako,utalilinda vipi soka lako lisishuke kiwango,utawezaje kudumu kwa muda mrefu kama Ronaldo, Modric, Zlatan, Buffon na wengine waliokipiga zaidi ya miaka 35. kila mtu anajua Bernard Morrisson ni mchezaji wa kiwango cha juu baada ya mechi ya jana, umewakumbusha hata wale walioanza kukusahu na kusema ufukuzwe Yanga,umewakumbusha wana Yanga na Watanzania ya kwamba una kitu kikubwa katika miguu na kichwa chako,Wana Yanga hawawezi kukukataa kama umeonyesha vitu vikubwa ulivyo navyo.Kila la heri Yanga inapoelekea kwenye Fainali za Kombe la Shirikisho barani Afrika,isiwe sherehe ni kufika fainali tu kama wenzetu walivyofika robo Fainali,lengo letu likawe ni kutwaa kombe hilo la Shirikisho barani Afrika.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.