Huyu jamaa asipoangalia ataachwa na yanga na simba pia ikampotezea,halafu akakosa nauli ya kurudi na akaanza mambo yake ya uwizi .
Mchezaji anamtishia mlinzi wa kambi na mwiko wa chuma,anabembelezwa na anachagua mechi ya kucheza,Kwa jicho lingine yanga walifanya la maana kumpa mkataba wa miezi 6,imagine kwa tabia zake hizo angesinya mkataba wa miaka miwili halafu achague mechi anayotaka na injury za visingizio au kuumwa.
Huyu Morison hafai kama ni mfupa haufai hata kwa supu,na msimwone ni mjinga kiasi hicho ,huyu jamaa inawezekana ana mishe zake za siri hapa bongo si kwa kujiamini kiasi hicho mbona kina Asante Nkwasi walikuwa na nidhamu na waliondoka mikono safi.
Mchezaji yuko ugenini anakimbia mechi ikiendelea anachukua bodaboda,huyu jamaa anajua chocho za bongo vizuri ,huyu jamaa ana mambo yake mbali na soka hawezi kuchezea chance kiasi hicho