Betting imenifanya masikini wa kutupwa

Betting imenifanya masikini wa kutupwa

Mbona kina sativa wanasema wanapata mamilioni ? Kina baba Levo?

Nishagundua betting sio ya masikini, tafuta odds 2 , stake high! Kaa hapo agiza kuku na balimi baridi !

Sio unaweka jero mkeka odds 250 unataka ushindi laki 5 !!!

Kingine betting niseme sio ajira, ama njia kuu ya kipato,,,ile ni kama changamsha bongo tu !
Usimdanganye mwenzako,hata hizo odds 2 ni ngumu kushinda
 
Habarini wana jamvi.

Sina mengi ya kuelezea ila hii issue ya BETTING tu, nimejitolea maeneo fulani na kwa mwezi naingiza 250K lakini nikiangalia maendeleo yangu tangu 2022 ni sawa na ziro, sina matumizi mengi kwa siku (hayazidi 4000/=) ila nimekuwa addicted na BETTING yaani siku haiishi bila kuweka mkeka.

Nimejikuta naingia kwenye madeni na kwa sasa nadaiwa zaidi ya 500K na watu watatu, huwa natamani kuacha ila wiki haikati narudi. Nilikuwa nimelenga kufungua studio/library mbili za kurusha movie na miziki lakini naona mwaka unaenda kuisha empty.

Deni lilianza kidogo tu ila nimekuwa na desire ya kulilipa kupitia BETTING. Nikipokea posho naweza kutumia hata laki kwa wiki nashinda lakini zote zinaishia hukohuko.

Naweza kuonekana wa ajabu lakini hii hali ndio napitia na inaniuma sana. Nimewakosea wazazi na majirani na Mungu lakini naamini huu utakuwa mwisho.

Nimeamua kwa sasa nijikite kwenykulipa madeni hayo japo naona naenda kudhalilika maana sina kitu kabisa na muda ndio huu.

Baada ya mwezi mmoja, yaani tar 30/06 nitakuja kutoa mrejesho, niombeeni ndugu zangu (seriously) niweze kuikwepa hii aibu.

Nisaidieni hata kwa ushauri wana Jf. Mwenyezi Mungu awabariki
Betting ni kubahatisha, unakaa chini ya mkungu ukisubiri udondokewe na embe. Wachache hutupiwa embe na wapita njia. Lakini kwa mtu alie pitia hesabu za probability ni nadra kubet.
 
Back
Top Bottom