Betting, michezo ya kubahatisha ni dhambi hata kama inaingizia nchi pesa nyingi

Betting, michezo ya kubahatisha ni dhambi hata kama inaingizia nchi pesa nyingi

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Naliomba Bunge tunapofikia kujadili ustawi wa jamii michezo ya kubahatisha toeni sauti Taifa linaangamia, hata kama Mwigulu anaona ni sawa tu kwa kuwa pesa inaingia, faida ya pesa inayopatikana na madhara ya michezo hiyo kwa Taifa ni ni sawa na tone.

Mwenyezi Mungu ameharamisha betting kwa nini tunafanya kiburi kufumbia macho suala hili, vijana wamekuwa walaibu Wachina wako kila kijiji wanawaibiwa watu innocent wasiojua, pesa ambayo ingewasaidia kulekebisha lishe ya watoto wetu wanaikomba na serikali ipo tu, tunaomba betting ipigwe marufuku. hakunaga utajiri wa kubahatisha. Mh. Rais na hilo nalo vipi?
 
Ko kamari ndo umeona dhambi ila ulawiti na ubakaji hujauona🤔 mashehe Kwa mapadri wanalawiti watoto wadogo huoni , dini yko imekataza kitimoto na unakula , wikiendi kunywa bia na kufanya ngono kinyume na maumbile afu huyohuyo anasema kamari dhambi😂 dah Kuna watu wanajichagulia dhambi Yani anachofanya yy sawa wanachofanya wengine dhambi
 
mwarobaini wa kamari ni vijana wawe na ajira. za kueleweka
90% ya wacheza kamari wanafanya hivyo kama plan B. baada ya kukosa ajira.
 
Hahaha ukiwa masikini utaambiwa wewe ni malaika, watakutumia watakavyo na utaona sawa tu, maana mliambiwa masikini ndio wataingia kwenye ufalme wa mbingu. Kama unaota amka tafuta maana ya neno DHAMBI kisha nenda katafute pesa.

Huko juu wanasema MONEY IS MONEY, haijalishi umepora, umeiba, umekaba au umeokota. Wewe unautafuta ufalme wa mbingu duniani?

Hata MWAMPOSA anatafuta pesa, amka kijana utatumika vibaya.
 
Back
Top Bottom