Betting ni biashara inayolipa, mpaka radio zimeamua kuachana na malengo ya msingi zimehamia huku. TCRA mpo kimya tu

Betting ni biashara inayolipa, mpaka radio zimeamua kuachana na malengo ya msingi zimehamia huku. TCRA mpo kimya tu

KARIBU TANZANIA: NCHI YA KAMARI! KAMARI! KAMARI!
 
EFM ndio waliooanza na MSHINDO
Clouds wakaiga na MCHONGO
Wasafi wakaingia kichwa kichwa na WASAFI BET... wakaona haitoshi wakaja na CHOTA MIHELA...

Jinsi wanavyopromot hadi aibu... Yaani ni njaa ndio yazidi...
Asee Ani mimi Huwa nazima kbs Radio nikiona inaongelea au kupromote mabeting hayo .. hasa EFM too much sana vipindi havinogi dakika tano 5 hao kuhamasisha utume 1000 ... Asee haya mambo haya....
 
RADIOs na TVs ila RADIOs Sana sana. Yaani ukifungua tu unakutana na tangazo la kamari. Kama zamani ilikuwa matangazo ya waganga wa kienyeji.

Sasa hivi Radio zimeamua zichezeshe zenyewe michezo hii. Hii biashara inaonekana kulipa sana.

Sijui tunatengeneza kizazi cha aina gani? Ukifungua hapa ni betting ukifungua chochote ni kamari tu. Watoto wanaokua wanajifunza nini?

Kwa maslahi ya kipato na kodi tunaharibu kizazi kijacho na cha sasa?

Yaani radio kwa siku. Content ni 20% ila BETTIN ni 80% where are we heading to?
Hili limeshaletwa hapa tena
 
Hili niliwahi toa maoni yangu Taifa limekuwa la kamari. Kila kona kila mahali kamari. Watu wanaibiwa tu pesa zao? mkuu..
 
Betting sio mbaya ila sasa inabidi bodi wafanye review ya sheria zao kwamba access ya michezo ya kamari ipatikane kwanzia mida ya jioni ili mtu aone uchungu wa kubetia ten aliyoitafuta the whole day
 
RADIOs na TVs ila RADIOs Sana sana. Yaani ukifungua tu unakutana na tangazo la kamari. Kama zamani ilikuwa matangazo ya waganga wa kienyeji.

Sasa hivi Radio zimeamua zichezeshe zenyewe michezo hii. Hii biashara inaonekana kulipa sana.

Sijui tunatengeneza kizazi cha aina gani? Ukifungua hapa ni betting ukifungua chochote ni kamari tu. Watoto wanaokua wanajifunza nini?

Kwa maslahi ya kipato na kodi tunaharibu kizazi kijacho na cha sasa?

Yaani radio kwa siku. Content ni 20% ila BETTIN ni 80% where are we heading to?
Mie pia nashangaa sana?
 
Kwa mtazamo wangu, bahati nasibu sio jambo baya kama zinachezeshwa kihalali; kwa maana ya kusajiliwa, na wachezeshaji hawaingilii mfumo (random selection of the system/machine, no bias). Mbona mataifa makubwa kama USA, UK, wanaendesha lottery kubwa kubwa kama shughuli zingine tu za kimaendeleo, ila they do not bias, na watu wanashinda kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Solutions watu wapewe elimu ya fedha...watanzania wengi hatuna elimu ya fedha na investment.
Nikiwa sekondari Mwalimu alituambia kuwa Bahati nasibu mnamchangia mtu Mmoja pesa.
Watu hawana elimu ya kupata fedha....lazima wabet Tu.
Ni reflection ya jamii yetu.
 
Kamari inalipa sana, just imagine Watu 50000 mmetoa elfu elfu, hapo ni pamoja na wanaocheza mara mbili au tatu na kuendelea...jumla mnakuwa mmechanga 50m...wanatoa milioni moja wanampa mmoja inayobaki ya kwao.

Hawawezi kufanya hayo bila baraka za Mamlaka, nadhani Mamlaka wao kikubwa ni wapate cha kwao kwa njia ya kodi au tozo n.k...na alimradi Mchezaji hulazimishwi.

Na kwa mifumo yetu corrupt usidhani hao Mamlaka wanaweza kuwazuia Wachezeshaji kufanya uhuni wao.

Ndio maana ukifuatilia baadhi ya michezo wataahidi kiwango fulani cha pesa alafu siku wanachezesha watakwambia Mshindi hajapatikana, ukweli ni kwamba lengo lao ndio halijafikiwa...kama kutoa milioni kumi kunataka wao wapate kwanza milioni mia moja ...basi kama haijafikiwa hawataitoa watakwambia Mshindi kakosekana.
 
Na huwa wanafurahi sana Mtu navyoshangilia kuwa wamempa milioni moja badala ya kumwambia ya kuwa awashukuru Wenzake waliomchangia.

Anayepata anapaswa kujua ya kuwa yupo aliyeacha kunywa chai asubuhi ndio yeye akapata hiyo milioni, yupo aliyeahirisha kununua dawa ndio yeye akapata milioni moja, yupo aliyetembea kilomita 10 kwa miguu ndio yeye akapata milioni moja.

Badala yake hizi Redio zinapokea shukurani zote wao binafsi na kukaa kimya makusudi zionekane zinawapa Watu pesa.
 
Back
Top Bottom