Kichwamoto
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 3,403
- 4,692
Hatari hatari hatari sanaRADIOs na TVs ila RADIOs Sana sana. Yaani ukifungua tu unakutana na tangazo la kamari. Kama zamani ilikuwa matangazo ya waganga wa kienyeji.
Sasa hivi Radio zimeamua zichezeshe zenyewe michezo hii. Hii biashara inaonekana kulipa sana.
Sijui tunatengeneza kizazi cha aina gani? Ukifungua hapa ni betting ukifungua chochote ni kamari tu. Watoto wanaokua wanajifunza nini?
Kwa maslahi ya kipato na kodi tunaharibu kizazi kijacho na cha sasa?
Yaani radio kwa siku. Content ni 20% ila BETTIN ni 80% where are we heading to?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Numbisa mimi nataka tuonane tafadhali, nimeshindwa kuvumilia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Inashangaza
Mwenye hiyo redio alishatangulia mbele za haki,kilichobaki ni kukosa muelekeo.Daaah Radio One Ndio Kabisa, Kuanzia Kipindi Chao Cha Kumekucha ni Matangazo ya Kamari Tu.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Tena hao wasafi FM ndo wanakera mno siku hizi, kiasi kwamba hata sports arena imepoteza mvuto, wanatumia muda mwingi kuchambua chota mihela badala ya mpira, wachambuzi wamegeuka mapromota wa kamari.EFM ndio waliooanza na MSHINDO
Clouds wakaiga na MCHONGO
Wasafi wakaingia kichwa kichwa na WASAFI BET... wakaona haitoshi wakaja na CHOTA MIHELA...
Jinsi wanavyopromot hadi aibu... Yaani ni njaa ndio yazidi...
Alafu hao hawajui hata kuprogram mambo yao... Kuna wakati wanasahau wanadhani wapo kwenye kipindi cha kamari na si michezo tena...Tena hao wasafi FM ndo wanakera mno siku hizi, kiasi kwamba hata sports arena imepoteza mvuto, wanatumia muda mwingi kuchambua chota mihela badala ya mpira, wachambuzi wamegeuka mapromota wa kamari.
Tatizo huwa zinachana hata utafute 1.02 hiyo ni labda under 5.5.....game inaisha 5-1 😆😆😄 mi nimefanya sana sema labda uzisome game na ubeti mara moja kwa wiki..Tafuta odds 1.20, three times a week..kila mkeka weka laki tano tano..faida ni laki 3 kwa @ wiki..Jiulize kama mangi dukan anapata faida ya 5000 ktk mauzo ghafi ya vocha za 100,000/= na hayo sio mauzo ya sku 1.