Ben-adam
JF-Expert Member
- Jun 2, 2023
- 1,043
- 2,309
Sidhani kama kuna mtu anabeti/alibeti kunishinda mimi!
Betting ina addiction ile mbaya, ikikukumba siyo rahisi kuacha.
Hongera nyingi kwa aliegundua hii michezo, alitumia akili kwelikweli! Nimetumia kila mbinu, kila hesabu ninazozijua lakini kipigo kiko palepale.
Pia niwape pole wale mnaoamini kwamba ipo siku watatusua kwenye Betting, mnajidanganya, mtaambulia hasara kiuchumi na kiafya. Namuona mtu mmoja anataka kusema ati "beti kwa starehe tu" "bet what you can afford to lose" pole sana.
Kadri unavyopoteza ndivyo unavyozidi kupambana ili uokoe ulichopoteza, aidha kwa kuongeza dau au odds. Wazee wa hizo kazi wananielewa. Kwasasa accounts zangu zote za kubetia nimeshazifunga japo kuna wakati nashawishika sana kufungua account mpya (addiction hiyo)najizuia.
Baadhi ya vitu vilivyofanya niamue kuachana na betting;
Nilikuwa napoteza muda mwingi hata wa kazi kutengeneza mkeka (uchambuzi)
Maumivu makali ya kihisia baada ya timu moja kunichania mkeka niliotumia muda mwingi kuutengeneza, (na hiyo timu iliyochana italaaniwa sana sana😮💨)
Niliona kabisa hapa nikiendelea hivi, presha na kisukari vile palee. Hakuna wakati mgumu kama pale timu uliyoipa ushindi inafikia dakika ya 70'au 80' ubao unasoma 0-0, mapigo ya moyo yanaenda mbio, umekaa tu cha ajabu unatokwa jasho kama vile unapanda mlima.
Ilifika hatua nikawa napumzika kwa muda mchache sana, muda wa kulala mimi niko live, siyo kwamba nachati wala nini, ni nabetika.
Hata ukinitumia ujumbe WhatsApp usitegemee kujibiwa, ukipiga simu kama sio mtu ambae namheshimu sana jibu ni moja tu "nitakupigia badae kidogo, nipe dakika tano" mpaka pale tukio ninalofuatilia litakapokamilika (tabia mbovu sana hii)
Leo nimemsikia mtu anasema anatafuta mtaji aanze kubeti😆😆 Kama hujawahi kubeti, wala usitake kujifunza.
Kweli betting ni haramu ni heri uraibu mwingine wowote ila sio betting/kamari, betting ni mufilisi janjaruka mapema.
Soma Pia: Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji