Betty Mkwasa: Fani ya Uandishi wa Habari ipo ICU kwa sasa na Nasikitika Wahusika tumenyamaza tu, huku ikienda Kufa kabisa

Betty Mkwasa: Fani ya Uandishi wa Habari ipo ICU kwa sasa na Nasikitika Wahusika tumenyamaza tu, huku ikienda Kufa kabisa

Asante sana kwa bandiko. Mwenye masikio na asikie. Wengi tulishaliona hili siku nyingi tangu kina Amina Chifupa (RIP) walipopewa mic za studio. Tukasema jamani utangazaji siyo sura wala umaarufu. Mambo yakazidi kuwa mabaya. Mara tukasikia mpaka kina Zembwela wamewekwa studio. Mara wazungumza kama cherehani kina Kitenge nao studio. Yaani Mkwasa kamaliza yote. Ukijua tu kupayuka au kuchekesha (wachekeshaji wengi wa bongo wanakasirisha badala ya kuchekesha) au sura nzuri unawekwa studio. Ndiyo maana tumekuwa na taifa lenye vijana hovyo kabisa.
Kitenge ni Mwandishi wa habari kabisa ila anajichetua tu.Alianzia Business times kwenye gazeti la Majira.
 
Maswali ya Kikuda na Kinafiki siyahitaji tafadhali sawa? Kawe nilihama tokea tarehe 18 February, 2024 na kuhamia Mapinga jirani kabisa na Marafiki zangu wa Kikosi Maalum Kiharaka na pia kuanzia tarehe 10 April, 2024 hadi leo hii ( hivi sasa ) nipo zangu Kampala Uganda hadi mwaka 2026 japo naweza kuendelea kuwepo hadi 2028 kama CDF Jenerali Muhoozi atakuwa Rais wa Uganda au Baba yake ataendelea hadi mwaka 2031.

Muhozi ndiye Rais baada ya Museveni,Wazee wa mambo ya rohoni tumeshaona kitambo,hilo halina shaka!
Tanzania pia 2025 Gwajima ajiandae kuchukua nchi!!
 
unatakiwa uogope sana nchi ambayo matumizi ni makubwa kuliko makusanyo na matumizi hayo yanafanyika kufumba macho ya watu watazamwao wafanye ujinga ili jamii ione ni sawa tu.....
ogopa nchi inayo pambania kusifia raisi wakati wananchi wana changamoto lukuki.... hata hawa wabunge wetu ni ma hopulesi tu
 
Kitenge ni Mwandishi wa habari kabisa ila anajichetua tu.Alianzia Business times kwenye gazeti la Majira.
Mkuu gazeti la Majira la lini? Majira ile ya zamani kabisa ndiyo ilikuwa gazeti lenye angalau viwango japo siyo sana. Baadae lilikuja kugeuka kuwa kama toilet paper tu. Ni kama Mwananchi iliyovurugwa sasa hivi. Kitenge zaidi ya kuzungumza kwa haraka haraka na kuweka mbwembwe kwenye habari za michezo, hakuna la ziada.
 
Ukiwaskiza wenye hizi media wanasema wao wanaangalia uwezo 'skills' wa mhusika kufanya kazi zao na wala sio ivo vyeti.

mtu anaweza kupanga vyeti kibao lakini asiwe na skills za kujieleza akaeleweka au akavutia wasikilizaji.

pesa ya media imekaliwa na hao wasikilizaji.

wasikilizaji wanapoongezeka na fuba linaongezeka ivoivo.
 
Maswali ya Kikuda na Kinafiki siyahitaji tafadhali sawa? Kawe nilihama tokea tarehe 18 February, 2024 na kuhamia Mapinga jirani kabisa na Marafiki zangu wa Kikosi Maalum Kiharaka na pia kuanzia tarehe 10 April, 2024 hadi leo hii ( hivi sasa ) nipo zangu Kampala Uganda hadi mwaka 2026 japo naweza kuendelea kuwepo hadi 2028 kama CDF Jenerali Muhoozi atakuwa Rais wa Uganda au Baba yake ataendelea hadi mwaka 2031.
Jibu swali ulilo ulizwa au kaa kimya, ni nani kuuliza histori yako uliyoitoa?
 
"Siku hizi Mtu akiwa tu ni Maarufu, Mchekeshaji, Msanii au Mbwabwaji Mitandaoni basi haraka sana anakuwa Mtangazi wa Redio na Tv. Naumia sana kuona hii Fani yenye Heshima kubwa duniani kote sasa hapa Tanzania ikiwa ipo ICU na Siku si nyingi inaenda Kufa kabisa. Sikatai ujio wa Teknolojia kwani hilo ni Jambo jema ila pamoja na Teknolojia lakini ile Misingi Mama ya Utangazaji / Uandishi wa Habari haijabadilika na wala haitokuja Kubadilika. Na kinachonisikitisha zaidi Sisi ambao ndiyo Wahusika tumenyamaza na wala hatuhoji hivyo kuendelea tu kuruhusu Upuuzi na Ukiukwaji mkubwa wa Kimaadili kuendelea kuwepo", amesema Mtangazaji Mkongwe, Mshindi wa Kike wa Afrika wa Tuzo ya Uandishi wa Habari za Ukimwi na Mweledi wa Tasnia Elizabeth ( Betty ) Mkwasa alipokuwa akizungumza na TBC1 katika Miaka 73 ya Utangazaji Tanzania.

GENTAMYCINE kila mara nimekuwa nikiisema hapa JamiiForums hii Tasnia ya Habari na Utangazaji halafu naonekana kama vile nina Nongwa nayo au nina Agenda nayo / nao Binafsi na wapo hadi Wanaonishutumu haya sasa leo kasema Mhusika mwenyewe hebu mbishieni basi na Yeye au Mshutumuni kama mfanyavyo Kwangu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE a.k.a Akili Kubwa na Tajiri wa Maono hakuna ambacho nakisema JF huwa hakiji Kutokea Ok?
Steve Nyerere mbion kupewa kipindi Crown fm
 
daah kuna wkt ilibaki kidogo nijitoe jf kwa akili ya kindezi km izi
Kwa nini hukujitoa? Mimi Gwajima (mchungaji) huwa namwita tapeli. Jamaa ni tapeli sana. Ila pamoja na utapeli wake nina uhakika anaweza kuwa ''mzuri'' kuliko Samia mara kumi. Pengine wewe unachanganya kuwa nimesema tumpe urais. La hasha. Mimi nimefananisha na Samia....au Magufuli.... hawa watu wawili tu.
 
Kitenge ni Mwandishi wa habari kabisa ila anajichetua tu.Alianzia Business times kwenye gazeti la Majira.
Kitenge ni Mwandishi wa Habari ila siyo Mwana Habari. Haya maneno Mawili Kitaaluma na kama Mbobezi tukuka kutoka SAUT Mwanza yana tofauti Kubwa mno japo najua wapo Wavivu wa Kufikiri watasema au watadhani ni sawa / yana fanana.

Tanzania ina Waandishi wa Habari ila Kenya ( Media ) ya Kenya ninayoikubali 100% ina Wana Habari.

Kula Madini haya Mkuu.
 
unatakiwa uogope sana nchi ambayo matumizi ni makubwa kuliko makusanyo na matumizi hayo yanafanyika kufumba macho ya watu watazamwao wafanye ujinga ili jamii ione ni sawa tu.....
ogopa nchi inayo pambania kusifia raisi wakati wananchi wana changamoto lukuki.... hata hawa wabunge wetu ni ma hopulesi tu
Thanks for nailing it Chief.
 
Jibu swali ulilo ulizwa au kaa kimya, ni nani kuuliza histori yako uliyoitoa?
Historia yangu hiyo nimeitoa kwa Fools wa mfano wako na Haters Wengineo waijue na nashukuru Sindano imeenda nilikotaka na ndiyo maana imekuuma na umekuja ukiwa na Hasira nayo.

Pole kwa Chuki, Hasira na Wivu ulionao ila ndiyo hivyo tayari Mwenyezi Mungu kanifungulia na atanifungulia zaidi mpaka tuheshimiane hapa JamiiForums.

Kudadadeki.... Na bado.....!!
 
Back
Top Bottom