Wana jamvini binafsi...sijawahi kuwa mpenzi wa Big Brother toka imeanzishwa..Najua yapo mazuri yanayoweza kupatikana kutoka katika Big Brother,lakini kuwepo kwa matendo mabaya ambayo hayafai kuonekana kwa TV kumenifanya nisivutiwe kabisa na Big Brother..Hawa dada zetu kwenda kwenye Big Brother na kufanya matendo ya ngono kunamaanisha nini? je kuna maanisha watanzania wanajivunia ngono? au ni tabia ya hawa wadada kuwachukulia hawa watu wanaokutana nao Big Brother matawi ya juu,hivyo wanalainika kulala nao ili pengine baada ya Big Brother anaweza kuwa amejipatia mwenza? au hapa Bongo hawapati wanaume hivyo wakienda Big Brother ndio hasa wanachokihitaji(top priority)?...Binafsi naona tabia hizi zinatuletea sifa mbaya kama taifa,na hata kama akienda mwanaume kule sioni sifa yoyote tunayoipata akishiriki ngono na mwanamke kutoka Taifa lingine...Kama ni hamu,zimalizeni kabla ya kwenda Big Brother mnaitangaza nchi yenu vibaya!!