Inna lillahi wa Inna ilayhi rajioon
May Allah Ta’ala grant her and all marhoomeen total Maghfirah and Jannatul Firdaus
May Allah Ta’ala grant all the bereaved Sabrun Jameel and Aafiyah
Aameen
Mama Fatma Karume, mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ameripotiwa kufariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 97.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Mama Fatma amefariki akiwa nyumbani kwa mmoja wa watoto wake huko Zanzibar.
Mama Fatma alikuwa mke wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Kifo chake ni msiba mkubwa kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Zanzibar, huku taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi na taratibu nyingine za msiba zikisubiriwa kutoka kwa familia au mamlaka husika.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama Fatma Karume mahali pema peponi.