Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BI. HALIMA MZEE MTOTO WA BI. TITI MOHAMED YOTE KAYAONA KWA MACHO YAKE
Picha hiyo hapo chini ni tawi la TANU lililofunguliwa na Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa mwaka wa 1954.
Ali Mshama katuachia hazina ya picha muhimu sana katika historia ya TANU.
Moja ya picha hizo ni picha hiyo hapo chini ya wanachama wa TANU wakiwa katika mkutano wa ndani akiwemo mtoto Halima labda ana umri wa miaka 10 hivi.
Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae Halima na baada ya mwanae ni Bi. Tatu biti Mzee.
Picha ya pili ni Bi. Halima Mzee kama alivyo hivi sasa.