Bi. Halima Mzee, mtoto wa Bibi Titi Mohamed yote kayaona kwa macho yake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BI. HALIMA MZEE MTOTO WA BI. TITI MOHAMED YOTE KAYAONA KWA MACHO YAKE

Picha hiyo hapo chini ni tawi la TANU lililofunguliwa na Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa mwaka wa 1954.

Ali Mshama katuachia hazina ya picha muhimu sana katika historia ya TANU.

Moja ya picha hizo ni picha hiyo hapo chini ya wanachama wa TANU wakiwa katika mkutano wa ndani akiwemo mtoto Halima labda ana umri wa miaka 10 hivi.

Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae Halima na baada ya mwanae ni Bi. Tatu biti Mzee.

Picha ya pili ni Bi. Halima Mzee kama alivyo hivi sasa.






 
Mzee wangu unatufundisha vyema historia, ila nina swali hiki chama cha Tanu hakikuwepo mikoa mingine ya Tanganyika?
Matola,
TANU ilikuwapo Tanganyika nzima.
 
Bibi Titi alikosea sana kutaka kumpindua Nyerere, Sijui nani alimpotosha, la sivyo angekuwa kiongozi mkubwa sana
 
Bibi Titi alikosea sana kutaka kumpindua Nyerere, Sijui nani alimpotosha, la sivyo angekuwa kiongozi mkubwa sana
Vito...
Bibi Titi Mohamed na Nyerere ugomvi wao ulianza ndani ya Halmashauri Kuu ya TANU mwaka wa 1963.

Ugomvi huu uliwajumuisha watu hawa wafuatao: Julius Nyerere, Suleiman Kitundu, Rajab Diwani na yeye Bi. Titi Mohamed.

Ugomvi ulikuwa kuhusu Aga Khan na uongozi wake katika East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

Bi. TIti na Nyerere wakatoleana maneno yasiyopendeza.
Kuanzia siku ile pakawa na chuki baina yao.

Hiki ni kisa kirefu nimekieleza chote katika kitabu cha Abdul Sykes.
Hilo la kupindua serikali ni 1969 hapa kati yalipita mengi katika uhasama wao.
 
Kwhy hiki kitabu kinapatikana wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…