Katika Nzengo yetu hususani kule juu wamo wateule wengi ambao wanaumizwa na hali ya mambo ilivyo sasa kwenye Kampuni ya walima.mboga mboga na kwenye Nzengo kwa ujumla.
Wamo wengi wanaounga mkono juhudi za upopoaji zinazofanywa na Mdunguaji aliyeko mafichoni dhidi ya Kunguru.
Taarifa za ndani kabisa zinabainisha kuwa mara baada ya Mkuu wa Nzengo aliyekuwepo kwenda safari ya mbali, Chekecheke alishika uongozi huku bi Kunguru akibaki kama boya tu.
Chekecheke ndiye mtoa amri na maelekezo kwa wateule wote ambapo hutoa maelekezo hayo kwa simu Moja kwa moja. Kati ya wateule hao wapo wanaotii mara moja, wapo wanaotii kwa Shingo upande na wapo ambao hawatii kabisa.
Inasemekana kuwa wateule ambao hawatii maelekezo ya chekacheka hukutana na rungu la kutupiwa virago. Ndio maana ya bandika bandua inayoendelea kwenye Nzengo.
Kwamba hata kwenye Uchafuzi ule, Bi Kunguru alikuwa ameandaa mtu wake kuwa mpambe, lakini Chekecheke aligoma na kumletea masharubu.
Kwamba, wiki tatu kabla ya mbio za Uchafuzi hazijaanza, Bi Kunguru alitaka kubwaga manyanga kutokana na marungu ya mdunguaji.
Ni Tyson, chips tamu, chekecheke.na viranja wawili wa zamani wanaosimamia rigwaride ndio walimzuia kwa hoja kwamba. Nzengo itavurugika na wote hawatakuwa salama akiwemo bi Kunguru mwenyewe!
Huko tuendako.mimi naona baadhi ya wateule wasiokubaliana na Nzengo kuongozwa na Chekecheke, wataacha kujificha, watajichomoa na kujiunga Moja kwenye Kampuni ya mdunguaji ambapo makao yao makuu yako kwenye pori Moja kule Bariadi. Ngoja tusubiri!