Hayuko sahihi kibiashara Azam Sport kibiashara inahusisha vitu vitatu uwanja wa Azam Complex,Azam Sports Tv Channels na Timu ya AzamKwa mujibu wa mtoto wake Abubakar Bakhresa, timu ya Azam inaendeshwa kwa hasara na inamuumiza sana mzee wake. Tafuta interview yake aliyofanya na UTV miaka 10 ya Azam Tv.
Kimahesabu kujua kuna faida au hasara inatakiwa kupiga hesabu vyote vitatu kama package moja
Uwanja Azam Complex ukiondoa timu maana yake unataka kuuua uvaki tu kama ukumbi wa kukodisha kama kumbi za harusi
Timu ni kama tu idara ya uendeshaji wa uwanja wa Azam Complex lakini pia akijenga timu vizuri aweza pata pesa nyingi kwa kuuza wachezaji timu zingine ndani na nje ya nchi na timu ikiwa nzuri akavuna pesa za ufadhili kutoka kwa wadhamini wengine wakubwa wa matangazo ya bidhaa zao
Atafute wataalamu wa nje wamsaidie kuijenga vizuri hiyo timu na mikakati gani ya kibiashara itumike kwa kupitia hiyo timu aingize pesa