Biashara 2 zinazomletea hasara Bakhresa

Biashara 2 zinazomletea hasara Bakhresa

Kwa mujibu wa mtoto wake Abubakar Bakhresa, timu ya Azam inaendeshwa kwa hasara na inamuumiza sana mzee wake. Tafuta interview yake aliyofanya na UTV miaka 10 ya Azam Tv.
Hayuko sahihi kibiashara Azam Sport kibiashara inahusisha vitu vitatu uwanja wa Azam Complex,Azam Sports Tv Channels na Timu ya Azam

Kimahesabu kujua kuna faida au hasara inatakiwa kupiga hesabu vyote vitatu kama package moja

Uwanja Azam Complex ukiondoa timu maana yake unataka kuuua uvaki tu kama ukumbi wa kukodisha kama kumbi za harusi

Timu ni kama tu idara ya uendeshaji wa uwanja wa Azam Complex lakini pia akijenga timu vizuri aweza pata pesa nyingi kwa kuuza wachezaji timu zingine ndani na nje ya nchi na timu ikiwa nzuri akavuna pesa za ufadhili kutoka kwa wadhamini wengine wakubwa wa matangazo ya bidhaa zao
Atafute wataalamu wa nje wamsaidie kuijenga vizuri hiyo timu na mikakati gani ya kibiashara itumike kwa kupitia hiyo timu aingize pesa
 
Wewe ndiyo muhasibu wake? Mimi natumia Azam pesa fresh ,umeme huku hadi wa mia 5 unanunua tofauti na mitandao mingine mpaka uwe na buku.

Timu ya Azam inapata matangazo ya biashara kutoka Azam ambayo ni very expensive kama angeilipa timu nyingine.
Kwa hiyo ni mtandao wa hoehae , kweli hapo ni hasara
 
Mbona na Mo alisema Simba nayo inamtia hasara? Mbona nayo haujaiweka? Biashara ambayo inahitaji sponsor ambayo hauuzi bidhaa ndivyo zinavyokuwa ,hao wanatoa huduma zina ups and down.

Kwa Azam Pesa ni matter of Time tu bado changa inapambana na ma-giants haiwezi kutoboa kwa uharaka.
Mkuu ujue tofauti ya Mo (Muhindi) na Bakhresa (Muarabu) ni kwamba Mo ni mbahili na siyo yeye tu nadhani unaujua ubahili wa wahindi kwenye biashara hata kwenye kulipa tu wafanyakazi wao ni mtiti, kinachofanya Mo watu wamkashifu hata akisema anapata hasara simba shida inakuwa siyo timu bali ni ubahili wake wa kushindwa kusajili wachezaji wazuri wa kuwavunjia mikataba toka kwenye timu kubwa, yeye anasubiri kuokoteza wachezaji ambao ni free agents ndio awasajili matokeo yake timu inaenda kwa kubahatisha tu

Lakini Bakhresa kwa namna anavyojitahidi kusajili wachezaji wazuri halafu timu inafanya vibaya shida inakuwa siyo yeye tena bali ni timu yenyewe na tatizo kubwa la azam linaweza kuwa ni kukosa mashabiki tu, maana timu ina kila kitu hadi uwanja wake lakini bado kuchukua ubingwa ni mtihani na ikienda kimataifa inaishia hatua za awali, yani bakhresa kwa wachezaji anaowasajili hawakustahili kuchezea timu kama azam laiti angekuwa anadhamini timu kubwa yenye mashabiki wengi kama simba au yanga kwa wale wachezaji basi ingefika mbali sana

Kuhusu azam pesa naweza kukubaliana na wewe bado changa ipewe muda lakini pale kwa timu ya azam hakuna cha uchanga tena bali kwa sasa ndipo uwezo wake ulipoishia, timu ina zaidi ya miaka ishirini tena ishawahi kuchukua hadi ubingwa wa ligi halafu mtu anasema eti iendelee kupewa muda, huko ni kujidanganya na hadi umesikia kwamba mzee mwenyewe kakiri hilo basi hata naye ameona kuna kitu anapoteza pale tofauti na matarajio yake na kile alichokiwekeza
 
Hizo zinapata hasara kati ya kampuni ngapi anazomiliki? Tuanzie kujua anamiliki kampuni ngapi
 
Kwani Azam anategemea biashara hizo pekee? Na mbona umeangalia upande mmoja,kwani faida ni ya kifedha pekee?. Kwa hapa alipofika Bakhresa kuwa na timu ni faida,hata MO au GSM nao wangetamani timu zile zingekua za kwao.Pia bado kuna nafasi ya timu ya Azam kufikia mbali hakuna haja ya kuikatia tamaa.Pia kuna biashara ya kuuza Wachezaji pia,kama vipi wanunue na kuuza kama kipaumbele ni pesa.
 
Back
Top Bottom