Habari. Katika uwanja wa usajili wa biashara(Tanzania's experience) kuna namna tofauti za unavyoweza kuamua ku'present biashara yako katika mamlaka za usajili wa biashara(BRELA). Sasa ukipeleka biashara yako ni lazma uwe na jina ambalo unahitaji kulitumia na muundo wa usaiji unaotaka kuufanya.
Kuna kusajili jina la biashara ambapo jina hilo linaweza kumilikiwa na kampuni iliyosajiliwa (mfano Mikoani Traders Limited anavyomiliki brand ama business name ya Azania, nk au Said Salim Bakhressa Company Limited inavyoweza kumiliki business name inayoitwa AZAM ICD)lakini pia jina la biashara linaweza kumilikiwa na mtu binafsi yaani wewe na TIN namba yako binafsi unaamua kusajili jina lako la kipekee ili ulitumie kuwakilisha biashara yako, na moja ya vigezo vya kusajili jina la biashara halipaswi kuwa na neno COMPANY ama LIMITED.
Namna ya pili ya usajili wa biashara ni kuwailisha biashara katika mamlaka za usajili wa biashara kama KAMPUNI. Katika kampuni kuna aina nyingi za kampuni lakini aina mbili zikiwa ndizo maarufu zaidi ambazo ni PRIVATE COMPANY LIMITED BY SHARES NA PUBLIC COMPANY LIMITED BY SHARES(PLC).
Sasa hayo majina ya Entreprises, Investiment, groups, traders, nk huwa mtu anayetaka kusajili huamua kuyaweka kulingana na dhima ama uhalisia wa picha ya biashara yake. Yana maana yake katika uhakisia japo inapokuja katika usajili watu wengi huwa hawazingatii maana zake bali huangalia tu namna jina lake litakavyokua likivutia maana hata mamlaka ya usajili hawajali lolote kuhusu maneno hayo. Kikubwa kinachozingatiwa ni kuwa katika kampuni NI LAZIMA JINA LIWE NA NENO LIMITED MWISHONI na katika majina ya biashara HAKUTAKIWI neno COMPANY wala LIMITED mwishoni mwa jina mzizi.
Mfano wewe unaitwa FORECASTER ina maana unaweza kusajili jina la biashara la FORECASTER ENTERPISES, FORECASTER TRADERS, FORECASTER INVESTMENT lakini pia unaweza kusajili kampuni ikaitwa FORECASTER ENTERPISES LIMITED, FORECASTER TRADERS LIMITED, FORECASTER INVESTMENT LIMITED, nk.
Endapo unahitaji kusajili kampuni, jina la biashara, trademarks, hivyo kuhitaji usaidizi katika documentation, TRA E-filing, drafting and online filing kwa gharama nafuu na haraka, usisite kuwasiliana nasi.
+255755963775 calls/WhatsApp
Tunapatikana Ilala Boma, Jengo la Mwalimu House ghorofa ya pili.