Biashara endelevu: Nini nini mtumizi na tofauti kati ya Kampuni, Entreprises, Investiment, groups na Limited (Ltd)

Zopo aina mbili za kampuni ambazo ni limited na unlimited,
1)limited ni kampuni ambazo zinasimama zenyewe pasipo kuingilia mmiliki,mfano kama itatokea shitaka mahakamani linalohusu kampuni, litahusu kampuni sio members,pia kama kampuni imekopa ama mazingira yoyote yanayo husu kutaifishwa mali basi mali zitakazohusika ni zile tu zenye usajili wa kampuni na si mali za members.Inaweza kushitaki ama kushitakiwa kama kampuni na si members wa kampuni.
2)unlimited ni kinyume chake,aina hii sio salama kwani kama kutatokea mazingira ya utaifishaji mali na thamani za mdeni hazija kamilika wataanza kukamata mali za members,
Usajili,
Andaa artical of association na memorandum kisha nenda brela.
Thnx
Namba Moja upo sahihi japo ningeenda ku qualify kidogo. Limited company zimegawanyika sehemu mbili, private limited company na public limited company na ndo aina za company pekee tulizonazo kwa sasa, unlimited liability company imeshafutwa kisheria.
 
Ni nini tofauti kati ya Majina haya yanapotumika katika baiashara mbalimbali: Kampuni, Entreprises, Investiment, groups, Limited (Ltd)
  • Nini Faida yake katika biashara
  • Utaratibu wake wa usajili
  • Utaratibu wake wa kikodi katika biashara
  • Changamoto zake katika biashara
Ok
 
Got you mkuu...asante. Mkurugenzi ni shahidi ktk any business deal done under his company, na sio police kupambana direct na kumshikilia mkurugenzi au meneja kuhusu ujinai au madai husika d
Mkuu naona kuna kitu hujanielewa naomba nirudie tena
1. KWENYE MASUALA YOTE YA MADAI hakuna mkurugenzi ambaye atawajibika kibinafsi bali ni kampuni itawajibika na mkurugenzi atakua ni shahidi tu
2. KWENYE MASUALA YA JINAI(Uhujumu uchumi mfano wale waliopewa tenda za ujenzi wa barabara wakashindwa kukamilisha, kugushi nyaraka, nk) hapo ndio mkurugenzi unaweza KUKAMATWA na kuwajibishwa individually
 
Habari. Katika uwanja wa usajili wa biashara(Tanzania's experience) kuna namna tofauti za unavyoweza kuamua ku'present biashara yako katika mamlaka za usajili wa biashara(BRELA). Sasa ukipeleka biashara yako ni lazma uwe na jina ambalo unahitaji kulitumia na muundo wa usaiji unaotaka kuufanya.
Kuna kusajili jina la biashara ambapo jina hilo linaweza kumilikiwa na kampuni iliyosajiliwa (mfano Mikoani Traders Limited anavyomiliki brand ama business name ya Azania, nk au Said Salim Bakhressa Company Limited inavyoweza kumiliki business name inayoitwa AZAM ICD)lakini pia jina la biashara linaweza kumilikiwa na mtu binafsi yaani wewe na TIN namba yako binafsi unaamua kusajili jina lako la kipekee ili ulitumie kuwakilisha biashara yako, na moja ya vigezo vya kusajili jina la biashara halipaswi kuwa na neno COMPANY ama LIMITED.
Namna ya pili ya usajili wa biashara ni kuwailisha biashara katika mamlaka za usajili wa biashara kama KAMPUNI. Katika kampuni kuna aina nyingi za kampuni lakini aina mbili zikiwa ndizo maarufu zaidi ambazo ni PRIVATE COMPANY LIMITED BY SHARES NA PUBLIC COMPANY LIMITED BY SHARES(PLC).
Sasa hayo majina ya Entreprises, Investiment, groups, traders, nk huwa mtu anayetaka kusajili huamua kuyaweka kulingana na dhima ama uhalisia wa picha ya biashara yake. Yana maana yake katika uhakisia japo inapokuja katika usajili watu wengi huwa hawazingatii maana zake bali huangalia tu namna jina lake litakavyokua likivutia maana hata mamlaka ya usajili hawajali lolote kuhusu maneno hayo. Kikubwa kinachozingatiwa ni kuwa katika kampuni NI LAZIMA JINA LIWE NA NENO LIMITED MWISHONI na katika majina ya biashara HAKUTAKIWI neno COMPANY wala LIMITED mwishoni mwa jina mzizi.
Mfano wewe unaitwa FORECASTER ina maana unaweza kusajili jina la biashara la FORECASTER ENTERPISES, FORECASTER TRADERS, FORECASTER INVESTMENT lakini pia unaweza kusajili kampuni ikaitwa FORECASTER ENTERPISES LIMITED, FORECASTER TRADERS LIMITED, FORECASTER INVESTMENT LIMITED, nk.

Endapo unahitaji kusajili kampuni, jina la biashara, trademarks, hivyo kuhitaji usaidizi katika documentation, TRA E-filing, drafting and online filing kwa gharama nafuu na haraka, usisite kuwasiliana nasi.

+255755963775 calls/WhatsApp
Tunapatikana Ilala Boma, Jengo la Mwalimu House ghorofa ya pili.​
Umeelezea vizuri sana mkuu.
Ila naomba kuuliza swali moja kwa ajili ya kuongeza uelewa zaidi.
Kwa mfano niko na duka langu nauza bidhaa kihalali kwa maana niko na Tin number na Leseni.
Sasa ninapokwenda tena Brela kusajili jina la biashara yangu ni nini manufaa/faida yake?
Na swali lingine nimeona kuna mahali umegusia kwamba kulikuwa na muundo wa kampuni japo umefutwa unaitwa Unlimited Liability company je hii ilikuwa ikoje na inafanyaje kazi?
 
Mkuu naona kuna kitu hujanielewa naomba nirudie tena
1. KWENYE MASUALA YOTE YA MADAI hakuna mkurugenzi ambaye atawajibika kibinafsi bali ni kampuni itawajibika na mkurugenzi atakua ni shahidi tu
2. KWENYE MASUALA YA JINAI(Uhujumu uchumi mfano wale waliopewa tenda za ujenzi wa barabara wakashindwa kukamilisha, kugushi nyaraka, nk) hapo ndio mkurugenzi unaweza KUKAMATWA na kuwajibishwa individually
Shukran sana kwa kutokuchoka kumuelewesha mdau. Naona mdau ni ima slow learner au alikuwa anajaribu kuvutia sheria impe favor upande wake.
 
Vema kabisa..no 2 hapo kwenye Jinai, nmeshaona mara kadhaa , kabla haijawa madai, mkurugenzi anakamatwa individually kwa kosa la jinai, labda la kimkataba baina ya mteja na kampuni, je hapo wapo sawa?, manake baada ya hekaheka inajulikana kuwa mteja anadai fidia au pengine kurejeshewa pesa ambayo mkataba ulishindikana..je hii haiingii kwenye ushauri no 1? (Tusaidiwe maslow learners)
 
Masuala ya kimkataba kimsingi huwa mashauri ya MADAI labda kwa uchache sana ukute inaangukia kwenye jinai. Ikitokea mkurugenzi amekamatwa kwa masuala ya kimadai ya kampuni ni eidha wakamataji hawajafuata/hawajui taratibu ama ni hujma amefanyiwa mkurugenzi.
 
Wanakamata kijinai..ila kule yakianza maelezo kukaonekana kulikuwa na mkataba ndo yanapogeuka madai ila tatizo mtu anakuwa ashasumbuliwa na zile hekaheka za police kulala ndani..sijui inakuwaga makusudi ya police au mhusika kutojua akiwa na mkataba uliovunjika anatakiwa aende wapi..mana akienda police wakiona ishu imekaa kipesa pesa wanaweza kushikilia kama jinai..hapo ndipo usumbufu
 
Habari. Katika uwanja wa usajili wa biashara(Tanzania's experience) kuna namna tofauti za unavyoweza kuamua ku'present biashara yako katika mamlaka za usajili wa biashara(BRELA). Sasa ukipeleka biashara yako ni lazma uwe na jina ambalo unahitaji kulitumia na muundo wa usaiji unaotaka kuufanya.
Kuna kusajili jina la biashara ambapo jina hilo linaweza kumilikiwa na kampuni iliyosajiliwa (mfano Mikoani Traders Limited anavyomiliki brand ama business name ya Azania, nk au Said Salim Bakhressa Company Limited inavyoweza kumiliki business name inayoitwa AZAM ICD)lakini pia jina la biashara linaweza kumilikiwa na mtu binafsi yaani wewe na TIN namba yako binafsi unaamua kusajili jina lako la kipekee ili ulitumie kuwakilisha biashara yako, na moja ya vigezo vya kusajili jina la biashara halipaswi kuwa na neno COMPANY ama LIMITED.
Namna ya pili ya usajili wa biashara ni kuwailisha biashara katika mamlaka za usajili wa biashara kama KAMPUNI. Katika kampuni kuna aina nyingi za kampuni lakini aina mbili zikiwa ndizo maarufu zaidi ambazo ni PRIVATE COMPANY LIMITED BY SHARES NA PUBLIC COMPANY LIMITED BY SHARES(PLC).
Sasa hayo majina ya Entreprises, Investiment, groups, traders, nk huwa mtu anayetaka kusajili huamua kuyaweka kulingana na dhima ama uhalisia wa picha ya biashara yake. Yana maana yake katika uhakisia japo inapokuja katika usajili watu wengi huwa hawazingatii maana zake bali huangalia tu namna jina lake litakavyokua likivutia maana hata mamlaka ya usajili hawajali lolote kuhusu maneno hayo. Kikubwa kinachozingatiwa ni kuwa katika kampuni NI LAZIMA JINA LIWE NA NENO LIMITED MWISHONI na katika majina ya biashara HAKUTAKIWI neno COMPANY wala LIMITED mwishoni mwa jina mzizi.
Mfano wewe unaitwa FORECASTER ina maana unaweza kusajili jina la biashara la FORECASTER ENTERPISES, FORECASTER TRADERS, FORECASTER INVESTMENT lakini pia unaweza kusajili kampuni ikaitwa FORECASTER ENTERPISES LIMITED, FORECASTER TRADERS LIMITED, FORECASTER INVESTMENT LIMITED, nk.

Endapo unahitaji kusajili kampuni, jina la biashara, trademarks, hivyo kuhitaji usaidizi katika documentation, TRA E-filing, drafting and online filing kwa gharama nafuu na haraka, usisite kuwasiliana nasi.

+255755963775 calls/WhatsApp
Tunapatikana Ilala Boma, Jengo la Mwalimu House ghorofa ya pili.​
Safi sana
 
Back
Top Bottom