Biashara gani halali inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa Siku?

Leseni ya broker ni Tsh 250000 tu unashindwa kukata hadi ukamatwe madini yachukuliwe na ufungwe au kupigwa faini ndo utatia akili
 
Usijifanye unajua wakati hujui 40yako ikifika utajuta kuifahamu serikali
Mkuu mimi kuhusu sheria hiyo nafahamu kidogo,ila kwa mantikihiyowachimbajiwadogo wote nchinzima wakamatwe wapewe adhabu, Naona itakuwa vizuri ili watu wote wawe na leseni
 
Mkuu mimi kuhusu sheria hiyo nafahamu kidogo,ila kwa mantikihiyowachimbajiwadogo wote nchinzima wakamatwe wapewe adhabu, Naona itakuwa vizuri ili watu wote wawe na leseni
Usiwaige wachimbaji kwa wewe mnunuzi ukikamatwa huna cha kujitetea we zoea tu 40 yako yaja
 
Leseni ya broker ni Tsh 250000 tu unashindwa kukata hadi ukamatwe madini yachukuliwe na ufungwe au kupigwa faini ndo utatia akili
Nielekeze kwa kipindi hiki ninachofanya hii biashara wapi nikachukue leseni. Naitaka sana. Utakuwa umenielewa.
 
Sure Mkuu
Hii biashara ni nzuri Ila ina changamoto hiyo..
 
Sure Mkuu
Hii biashara ni nzuri Ila ina changamoto hiyo..
 
Naunga mkono hoja, nafanya hii tena kwenye ka site kadogo tu ila inanitoa fresh na nilianza na ka mtaji kadogo.
Mkuu na Mi nipo kwny mchakato Wa kufungua mgahawa kuna vitu muhimu nahitaji kujua VP nije pm?
 
Ungesoma convo za nyuma ungeelewa,.kuna mtu alibisha kua huwez tengeneza profit ya lak3 kwa baishara ya mtaj mdogo,et had uwe na kuanzia 50mil au 60mil,mi ndo nkamjib hivyo aende akamuulize edo pale
Mkuu, ukweli ni kwamba watu wanaishi maisha ya kuigiza ..binafsi nilishhawah kuongea na edo aise anyway mkuu watu wabishi unawaacha tu
 
Ngoja na mimi nitie neno kidogo hapa.

Ukubwa wa faida kwenye biashara unategemea mambo mawili makubwa..
1/Ukubwa wa Mtaji.
2/Mzunguko wa biashara.

Kwa mtaji wa Milioni kumi tu, maana yake huo mtaji mdogo, sio rahisi kutengeneza faida ya shilingi Laki tatu kwa siku. Haiwezekani kabisa. Kwa kanuni za kibiashara faida ya juu kabisa ya mtaji wako kwa siku sio zaidi ya 1% ambapo kama mtaji wako ni milioni kumi faida ya juu sana unayoweza kutengeneza kwa siku haiwezi kuzidi shilingi laki moja.

Na kama utataka kutengeneza faida kubwa kwa kutumia mzunguko wa kibiashara basi hiyo milioni kumi inaweza kuleta faida ya laki tatu kwa siku LAKINI ni biashara chache sana, katika mazingira yenye watu wengi na kwa muda maalum inaweza kukuingizia faida hiyo kama Mgahawa wa Chakula, Duka la vyakula, Genge katika Soko nk.

Usisahau pia penye faida na hasara ipo nje nje. Hivyo uwe tayari pia kutengeneza hasara ya kiasi hicho hicho katika mazingira ya biashara ya namna hiyo.
 
Pia kuhusu biashara ya madini hapa Tanzania, unapaswa kujua mambo haya pia yameizunguka biashara hiyo.
1/Ubabaishaji.
2/Utapeli.
3/Ujanja.
4/Kubahatisha.

Ni vyema ukajifunza vizuri na kujitathmini ili kuona kama utaiweza kabla ya kutumbukiza mtaji wako kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…