Biashara gani halali inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa Siku?

Biashara gani halali inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa Siku?

Biashara yoyote ile ina faida. Ni namna ya kuweka strategies na location nzuri basi.
Mkuu hii kauli Siku za nyuma nilikuwa ninaidharau, lakini ina maana kubwa sana.

Kuna siku nilikuwa ninaangalia video ya speaker mmoja wa TED x talks.

Jamaa alianza kutoa mifano mingi ya business ideas ambazo mwanzo utawanza haiwezekani lakini kwa kufikiri creatively akatoa posible alternatives.

Jamaa ni mjasiriamali lakini alinisaidia sana hadi sasa kutekeleza mambo yangu na kutatua matatizo yangu.
 
Umeenda mbali sana, ukiwa mnunuzi wa dhahabu mbichi unahitaji mzani tu, labda laki mbili. Dah sijue nifafanue vp.


Tufanye ana 5m.

1g of gold=65,000Tsh
5m/65,000=76.92g
Ubora/purity=86%
Bei=86,000Tsh kwa wenye leseni
Mauzo=76.92g*86%*86,000=5,689,230,

Hata ukipandilia bei akanunua kwa 70 au 72 bado anapata hiyo faida
Nakuelewa sana Mkuu sababu mim mwenyewe , nipo hapa mitaa ya GEITA hiyo milioni 9 inatosha sana.
 
Wakuu mimi ni mjasilimali mdogo tu ambae kwa siku naweza tengeneza faida ya kuanzia elfu 30 or elfu 40. Sasa kwa sasa natafuta biashara ambayo inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa siku.Na vimiradi viwili ambavyo vinaniingizia hiyo pesa.

Mtaji uliopo ni kati ya (9/12 Million).Hii biashara nahitaji niisimamie mie mwenyewe.

Nimejitahidi kusoma forex, BTC lakini naona kichwa changu ni kigumu kuelewa .

Napokea ushauri wowote ila isipokuwa wa kuwekeza kwenye kilimo. Na pia wa kufanya biashara ya kushirikiana na mtu(kugawana share).

Karibuni kwa mawazo.
Tafadhari mimi naomba unifahamishe hiyo shughuri inayokuingizia elfu 30-40 kwa siku
 
Hiyo 50000 bila shaka ni mauzo! Hapo faida (baada ya kuondoa gharama) ni sh ngapi? Kumbuka chakula chako, na gharama ya muuzaji hata kama ni mwenyewe ni sehemu ya gharama!
Muwa mmoja shambani ni Tsh.200-300, huo muwa mmoja unatoa vifuko 2 mpaka 3. Kula mchana cyo lazima kikubwa asubuhi kula kama mfalme mchana kunywa maji kama mtumwa kisha piga kazi
 
Mkuu watanzania wengi wanafeli kwa kuogopa kujaribu. Nimejaribu kufuatilia maelezo yako, inaonyesha kwa dhati ya moyo wako umejitoa kusaidia lakini kwa ugumu wa watu wanaogopa kujaribu ni kama unampigia gitaa mbuzi. Mimi nitakutafuta inbox mkuu ili unielekeze vzr japo sie niliyeomba ushauri, lakini naona ufahamu wako unaweza kusaidia watu humu.
[emoji121]
NA HIVI NDIVYO WANAVYODUFULIWA WATU KIURAHISI!!!
 
Umeenda mbali sana, ukiwa mnunuzi wa dhahabu mbichi unahitaji mzani tu, labda laki mbili. Dah sijue nifafanue vp.


Tufanye ana 5m.

1g of gold=65,000Tsh
5m/65,000=76.92g
Ubora/purity=86%
Bei=86,000Tsh kwa wenye leseni
Mauzo=76.92g*86%*86,000=5,689,230,

Hata ukipandilia bei akanunua kwa 70 au 72 bado anapata hiyo faida
Dhahabu kama uzifahamu vizur itakula kwako
 
Mkuu saluni mbili zote kwa pamoja nachukua laki na 60 kwa wiki.Kiduka ndio kinaniletea hiyo faida 30/40 sema pesa ya saluni huwa siitumii kwa shughuri yeyote hii baada yakuiweka ndio imeleta hio pesa 9/12M.Kiduka nakitumia kuendeshea maisha yangu nandio kinatengeneza hiyo pesa 30/40 per day.
Saloon za like au za kiume Mkuu?
Sio Rahisi kama ulivyo andika
 
Hii yangu ni kiduka cha nafaka tu, yaan nauza mchele,sukari, ngano, sembe, dona na soda.
Ila ka site kamezungukwa na mama ntilie kibao na hao ndio wateja wangu wakubwa.
OK ahsante nashukuru
 
unatosha sana kwa dhahabu wala sio mdogo unaweza ukaanza hata kwa laki mbili issue ngumu kwenye dhahabu ni kuifahamu dhahabu yenyewe...lindi kuna maeneo unapata dhahabu hadi 45 elfu kwa Gram na unaweza kuiuza hapo hapo kwa 65-80 elfu
nipe ramani
 
Mi nafikiri faida ya biashara inavary siku to siku kulingana na demand ya wateja, io ya kusema laki tatu kwa siku kwani unajiuzia mwenyeme
Kwani mkuu ulisikia mtu anapata faida ya elfu kumi kwa siku anakuwa anajiuzia mwenyewe?.
 
unatosha sana kwa dhahabu wala sio mdogo unaweza ukaanza hata kwa laki mbili issue ngumu kwenye dhahabu ni kuifahamu dhahabu yenyewe...lindi kuna maeneo unapata dhahabu hadi 45 elfu kwa Gram na unaweza kuiuza hapo hapo kwa 65-80 elfu
Mwaga Nondo mkuu
 
Watu wengi humu tunaropoka tu kuhusu biashara lakini kiuhalisia wengi wetu hatuna hata biashara ya mtaji wa genge la nyanya.

Mleta mada ameweka wazi kabisa kuwa..
1/Anao mtaji wa shilingi milioni 9-12.
2/Anataka kupata faida ya shilingi Laki tatu kwa siku.

Tuwe wakweli na wawazi, hicho kitu kiujumla hakiwezekani katika mazingira ya kawaida ya kibiashara nyingi hapa Tanzania labda iwe ni mambo ya bahati nasibu, kubet na kupiga dili tata.

Kwa mfano mtu anasema akanunue madini machimboni ili kuja kuyauza mjini. Kwa mtaji wa milioni 10, maana yake atanunua dhahabu ya milioni 10 na kuweza kuja kuiuza milioni 15 kwa makisio ya juu sana(kitu ambacho sio rahisi pia), hivyo faida ni milioni tano. Lakini hiyo sio bidhaa ya kuuzwa kama nyanya ambapo kila siku watu watanunua, na hupitia mchakato mrefu huku ikitumia siku kadhaa na mnyororo wa wafanyabiashara kadhaa. Hivyo faida ya laki tatu kwa kila siku hiyo ni hadithi pia.
 
Back
Top Bottom