Biashara gani halali inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa Siku?

Biashara yoyote ile ina faida. Ni namna ya kuweka strategies na location nzuri basi.
Mkuu hii kauli Siku za nyuma nilikuwa ninaidharau, lakini ina maana kubwa sana.

Kuna siku nilikuwa ninaangalia video ya speaker mmoja wa TED x talks.

Jamaa alianza kutoa mifano mingi ya business ideas ambazo mwanzo utawanza haiwezekani lakini kwa kufikiri creatively akatoa posible alternatives.

Jamaa ni mjasiriamali lakini alinisaidia sana hadi sasa kutekeleza mambo yangu na kutatua matatizo yangu.
 
Nakuelewa sana Mkuu sababu mim mwenyewe , nipo hapa mitaa ya GEITA hiyo milioni 9 inatosha sana.
 
Tafadhari mimi naomba unifahamishe hiyo shughuri inayokuingizia elfu 30-40 kwa siku
 
Hiyo 50000 bila shaka ni mauzo! Hapo faida (baada ya kuondoa gharama) ni sh ngapi? Kumbuka chakula chako, na gharama ya muuzaji hata kama ni mwenyewe ni sehemu ya gharama!
Muwa mmoja shambani ni Tsh.200-300, huo muwa mmoja unatoa vifuko 2 mpaka 3. Kula mchana cyo lazima kikubwa asubuhi kula kama mfalme mchana kunywa maji kama mtumwa kisha piga kazi
 
[emoji121]
NA HIVI NDIVYO WANAVYODUFULIWA WATU KIURAHISI!!!
 
Dhahabu kama uzifahamu vizur itakula kwako
 
Saloon za like au za kiume Mkuu?
Sio Rahisi kama ulivyo andika
 
Hii yangu ni kiduka cha nafaka tu, yaan nauza mchele,sukari, ngano, sembe, dona na soda.
Ila ka site kamezungukwa na mama ntilie kibao na hao ndio wateja wangu wakubwa.
OK ahsante nashukuru
 
unatosha sana kwa dhahabu wala sio mdogo unaweza ukaanza hata kwa laki mbili issue ngumu kwenye dhahabu ni kuifahamu dhahabu yenyewe...lindi kuna maeneo unapata dhahabu hadi 45 elfu kwa Gram na unaweza kuiuza hapo hapo kwa 65-80 elfu
nipe ramani
 
Mi nafikiri faida ya biashara inavary siku to siku kulingana na demand ya wateja, io ya kusema laki tatu kwa siku kwani unajiuzia mwenyeme
Kwani mkuu ulisikia mtu anapata faida ya elfu kumi kwa siku anakuwa anajiuzia mwenyewe?.
 
unatosha sana kwa dhahabu wala sio mdogo unaweza ukaanza hata kwa laki mbili issue ngumu kwenye dhahabu ni kuifahamu dhahabu yenyewe...lindi kuna maeneo unapata dhahabu hadi 45 elfu kwa Gram na unaweza kuiuza hapo hapo kwa 65-80 elfu
Mwaga Nondo mkuu
 
Watu wengi humu tunaropoka tu kuhusu biashara lakini kiuhalisia wengi wetu hatuna hata biashara ya mtaji wa genge la nyanya.

Mleta mada ameweka wazi kabisa kuwa..
1/Anao mtaji wa shilingi milioni 9-12.
2/Anataka kupata faida ya shilingi Laki tatu kwa siku.

Tuwe wakweli na wawazi, hicho kitu kiujumla hakiwezekani katika mazingira ya kawaida ya kibiashara nyingi hapa Tanzania labda iwe ni mambo ya bahati nasibu, kubet na kupiga dili tata.

Kwa mfano mtu anasema akanunue madini machimboni ili kuja kuyauza mjini. Kwa mtaji wa milioni 10, maana yake atanunua dhahabu ya milioni 10 na kuweza kuja kuiuza milioni 15 kwa makisio ya juu sana(kitu ambacho sio rahisi pia), hivyo faida ni milioni tano. Lakini hiyo sio bidhaa ya kuuzwa kama nyanya ambapo kila siku watu watanunua, na hupitia mchakato mrefu huku ikitumia siku kadhaa na mnyororo wa wafanyabiashara kadhaa. Hivyo faida ya laki tatu kwa kila siku hiyo ni hadithi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…