unachosema ni kweli kabisa,mwaka juzi nilishawishika kuifanya hiyo biashara kwa kufuata maneno ya watu kama hivi,nikapata mtu mzoefu akanipeleka huko porini,kukusanya kiasi unachotaka sio kazi ya siku moja na sio kila mtu tu anauziwa,mazingira ya huko porini ni machafu na ikibidi ulale huko unalala chini kwenye mahema ya maturubai kuna tents kama zile za wakimbizi....mazingira ni mabaya mno ,nilikutana na michana ambaye ilikua anatembea na madigala ili wamkusanyie mzigo mapema ili asikae sana porini...na kuhusu bei ni kweli haina tofauti sana na bei ya dunia,na kuna siku anakuja mtu au watu wametumwa mzigo mkubwa na wahindi wanapandishA bei na kila mchimbaji anawauzia wao...profit margin inakua finyu mnoo kiasi kwamba anayenunua mzigo mkubwa ndo ataiona hiyo faida per gram....Hiyo dhahabu mbichi huwezi kuipata kijingajinga tz hii kwa miaka hii kila wanapochimba kuna wanunuzi ambao ndio wafadhili wao we kama hufadhili uchimbaji dhahabu labda upate ya wizi