Biashara gani naweza kufanya kwa mtaji wa laki nane katika mji wa Kahama?

TRABSOH

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
351
Reaction score
559
Wakuu habari,

Natumai kuna wajuzi na wenye uzoefu na mji wa kahama kwenye eneo la ujasiriamali hapa, nina ichi kiasi cha laki nane ambacho natamani kisikae kizalishe chochote kitu ili nitanue wigo wa mapato yangu ata kwa kidogo.

Naomba mawazo yenu wakuu.

Asante
 
wakuu mnaitwa huku@leejay4@mideko@antonnia๐Ÿค“
 
Kwa hapo kahama mjini kuna maduka mengi ya jumla hapo kariakoo ndogo stendi kwa chini kwanini usifungue kioski upande wa mtaa wa idara maji nyuma huku karibu na shule ya msingi na sekondari hamna maduka mengi kule mpaka ufike royal food ndiyo kuna maduka weka vitu vichache kwenye shelf na chini weka kilo 25 unga mchele mafuta kupikia anza na 10 Lt kwakuwa eneo lile ni karibu na shule weka juice ndogo ndogo pipi nyingi na chokoleti ndogo
 
Asante mkuu
 
Jaribu kutembelea Mhongolo hasa mtaa wa Nyashimbi pana soko jipya ndo limeshika kasi pale.

Fremu ni bei nafuu kuliko mjini na population si haba,watu ni wengi tu.
 
Oya njoo mhungula mitaa ya maleba hapa kuna fursa nyingi tu
 
mbona pale hakuna secondary mkuu ila kunashule yamsingi tu
 
Ni vizuri kusikia kuwa una hamu ya kuendeleza kipato chako kupitia ujasiriamali. Hapa kuna baadhi ya mawazo ambayo unaweza kuzingatia ukiwa Tabora:

  1. Kilimo: Unaweza kuanzisha shamba dogo au bustani ya mboga ambayo itakupa fursa ya kuzalisha mazao kwa ajili ya matumizi yako na kuuza ziada. Unaweza pia kujaribu kilimo cha kibiashara kama vile ufugaji wa kuku au ng'ombe wa maziwa.
  2. Biashara ndogo-ndogo: Fikiria kuanzisha biashara ndogo-ndogo kama kuuza bidhaa za rejareja, kama vile vyakula, vinywaji, au bidhaa za nyumbani. Unaweza pia kufikiria kutoa huduma kama vile ufungaji wa simu au ukarabati wa vifaa vya umeme.
  3. Huduma za usafiri: Ikiwa una gari au pikipiki, unaweza kuzingatia kutoa huduma za usafiri kama vile usafiri wa abiria au usafirishaji wa mizigo ndani ya jiji au mkoa.
  4. Ufundi na huduma za kibunifu: Kama una ujuzi katika eneo fulani kama ufundi wa umeme, ujenzi, au uchongaji, unaweza kutoa huduma zako kwa watu katika eneo lako.
  5. Biashara ya mtandaoni: Unaweza kuanzisha biashara ya mtandaoni kama vile kuuza bidhaa kupitia jukwaa kama Jumia, Kilimall, au kuanzisha duka lako la mtandaoni. Pia, unaweza kutoa huduma za kipekee au ufundi kwa njia ya mtandaoni.
Kabla ya kuanza biashara yoyote, ni muhimu kufanya utafiti wa soko, kuandaa mpango wa biashara, na kuzingatia masuala ya kifedha na usimamizi. Pia, unaweza kutafuta msaada kutoka kwa wataalamu wa biashara au mashirika yanayosaidia wajasiriamali katika eneo lako.
 
Chatgpt uyu miyeyusho anatoa mawazo general haangalii mazingira wala wakati
 
kuuza ๐‚๐‡๐”๐๐ˆ ๐ณ๐š ๐ค๐ข๐ค๐ž ๐ฏ๐ข๐š๐ญ๐ฎ, ๐Œ๐ฉ๐ž๐ฌ๐š, ๐ค๐ฎ๐ฌ๐š๐ฃ๐ข๐ฅ๐ข ๐ฅ๐š๐ข๐ง๐ข, ๐ฏ๐ข๐š๐ญ๐ฎ ๐ฏ๐ฒ๐š ๐ค๐ข๐ค๐ž, ๐ฌ๐จ๐ค๐ฌ๐ข,

๐ง๐š๐ค๐š๐ณ๐ข๐š ๐ฎ๐ค๐ข๐ฎ๐ณ๐š ๐œ๐ก๐ฎ๐ฉ๐ข ๐ณ๐š ๐ค๐ข๐ค๐ž ๐ฎ๐ญ๐š๐ฉ๐ข๐ ๐š ๐ฆ๐ค๐ฎ๐ฎ ๐ง๐š ๐Ÿ๐š๐ข๐๐š ๐ฎ๐ญ๐š๐ข๐จ๐ง๐š. ๐”๐ค๐ข๐š๐ง๐ณ๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ก๐ข๐ฒ๐จ ๐›๐ข๐š๐ฌ๐ก๐š๐ซ๐š ๐ง๐ข๐ฉ๐ž ๐ฆ๐ซ๐ž๐ฃ๐ž๐ฌ๐ก๐จ
๐ฆ๐ข๐ฆ๐ข ๐ง๐ข๐ฅ๐ข๐ข๐Ÿ๐š๐ง๐ฒ๐š ๐ข๐ค๐š๐ง๐ข๐ฅ๐ข๐ฉ๐š ๐ฅ๐š๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ง๐ข๐ฅ๐ข๐ค๐ฎ๐š ๐ง๐š๐๐ข๐ง๐๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ค๐ข๐ฅ๐š ๐ฌ๐š๐š ๐š๐ค๐ข๐ฃ๐š ๐ฆ๐ฐ๐š๐ง๐š๐ฆ๐ค๐ž ๐ค๐ฎ๐ง๐ฎ๐ง๐ฎ๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ฎ ๐ค๐ฎ๐ง๐š ๐ค๐š๐ฉ๐ข๐œ๐ก๐š ๐Ÿ๐ฎ๐ฅ๐š๐ง๐ข ๐ค๐š๐ง๐š๐ง๐ข๐ฃ๐ข๐š ๐ฃ๐ข๐ง๐ฌ๐ข ๐ข๐ญ๐š๐ค๐š๐ฏ๐ฒ๐จ ๐ฆ๐Ÿ๐ข๐ญ๐ข.
 
Asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ