Biashara gani naweza kuiganya kwa mtaji wa 2M

Biashara gani naweza kuiganya kwa mtaji wa 2M

Sawa mtaa hauhitaji degree.

Umeshindwa kufikiria kupitia maarifa uliyoyapata shule

Umesoma uchumi na fedha concept ya DEMAND and SUPPLY ilielewa vizuri. Je umeshindwa kuiapply hapo unapoishia ukajua which is which!?

Tumia hio shahada kujiongeza
Boss, Kuuliza ili afahamu kutoka kwa walio field haimaanishi kwamba hatotumia hiyo elimu.
Hii speech acerbity unayotumia kwake haina ulazima.
 
Msominwa uchumi hawezi hata fanya analysis kujua ni biashara Gani itamfaa kwa huo mtaji. Aisee. Elimu yetu hii sijui ina faida Gani.
Kuuliza ni moja ya analysis pia. Anafanya utafiti mwepesi. Au alitakiwa asiulize lolote aanze tu biashara kwa kutumia theory alizosomea na uzoefu hana?

Kijana kamaliza shule, kaamua ajiajiri asikae tu kusubiri ajira, alitakiwa kwanza apongezwe kwa hayo mawazo, Kuanza kuponda elimu aliyonayo haina msaada kwake. Kama una lolote la kumjenga, mwambie.
 
Moshi/Moro mkungu sh ngapi?

Usafiri toka Moshi/Moro mpaka dar kiasi Gani?

Dar mkungu sh ngapi?

Bei zinatofautiana kulingana na ukubwa, aina na upatikanaji wa ndizi, kuna kipindi zinapanda na msimu mwengine zinapungua bei. Ndio maana ni muhimu kufanya utafiti kujua bei na kujua unamletea nani mzigo wako.

Kuna jamaa wanachukua mzigo usiku, asubuhi wanauza Mabibo na kugeuza kwenda kukusanya tena, usiku wanalala trna kwenye mabasi.

Morogoro kuna sehemu wanaita Singisa au Rumba chini, mnada Jumapili asubuhi, wanaleta ndizi hapo na mazagazaga kibao kutoka Rumba juu, ni mwendo wa kunapatana, kununua, kukusanya mzigo, kunakua na malori kuleta Dar, unashirikiana na wenzako, yanaleta Buguruni.
 
Kwanza sahau kabisa kama una mtaji wa kiasi fulani. Angalia fursa zilizopo eneo unaloishi, fanya utafiti wa mambo yote muhimu kama upatikanaji wa mzigo, location, namna utasambaza, fungu la emergency n.k halafu angalia ni mtaji gani utatosha, kama itazidi kidogo fikiria utajazia vipi, husi-limit akili hapo hapo kwenye kiasi ulichonacho tu. Nilichojifunza kwenye biashara inabidi wazo la biashara litangulie kabla ya mtaji ili hela ikipatikana tu unaingia mzigoni. Ila hela ya mtaji ikipatikana kabla ya wazo kile kipindi ambacho unafikiria ufanye nini hela itaisha katika mazingira ambayo uelewi elewi imekuaje. Kama unaishi karibu na barabara kuu tafiti eneo ambalo magari yanapita pita pia na jirani na ofisi na makazi ya watu wenye usafiri binafsi fungua car wash 1.5 milion inatosha. Pia kama una kipaji au kipawa chochote mfano utangazaji, ubunifu wa mavazi, hodari kwenye mchezo fulani, uhandishi n.k usidharau jiendeleze mdogo mdogo kwa kufanya short course, kujifunza zaidi mitandaoni n.k hakuna anaejua kesho uenda kipaji au kipawa chako ndo kikaja kukutoa kimaisha.
 
Bei zinatofautiana kulingana na ukubwa, aina na upatikanaji wa ndizi, kuna kipindi zinapanda na msimu mwengine zinapungua bei. Ndio maana ni muhimu kufanya utafiti kujua bei na kujua unamletea nani mzigo wako.

Kuna jamaa wanachukua mzigo usiku, asubuhi wanauza Mabibo na kugeuza kwenda kukusanya tena, usiku wanalala trna kwenye mabasi.

Morogoro kuna sehemu wanaita Singisa au Rumba chini, mnada Jumapili asubuhi, wanaleta ndizi hapo na mazagazaga kibao kutoka Rumba juu, ni mwendo wa kunapatana, kununua, kukusanya mzigo, kunakua na malori kuleta Dar, unashirikiana na wenzako, yanaleta Buguruni.
Aise naweza kuja pm tuyajenge mkuu
 
Back
Top Bottom