Biashara gani ndogo inayoweza niingizia hata 10,000 kwa siku?

Biashara gani ndogo inayoweza niingizia hata 10,000 kwa siku?

Boanerge

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
686
Reaction score
180
Habari wanajamvi,

Nataka kuanzisha biashara ila sijui ni biashara gani maana mimi ni mwajiriwa na nataka hiyo biashara walau inihakikishie faida ya 5,000 mpaka 10,000 kwa siku. Mtaji wangu ni 1,000,000/=

Naombeni mawazo yenu.
 
Inategemea mradi wako, na biashara ndogo kwako ina maana ipi....

Kwa mfano nina weza kufungua gym bubu ikawa inaingiza pesa hiyo kila siku. Lakini mtaji wake ukawa ni 1 mil kwenda mbele. Sasa sijajua kama kwako hii itakuwa ni biashara ndogo ama kubwa.
 
Habari wanajamvi,

Nataka kuanzisha biashara ila sijui ni biashara gani maana mimi ni mwajiriwa na nataka hiyo biashara walau inihakikishie faida ya 5,000 mpaka 10,000 kwa siku.

Naombeni mawazo yenu.
Biasharay kuchoma mahindi ni biashara ambayo watu wanaidharau lakini ukichoma mahindi 100, unapata 30,000 bila chenga. Gharama ni ndogo tu na mtaji wake ni: (1) jiko =20,000
(2) mkaa =8,000 (3) mahindi 100=300-400@=30,000-40,000
(4) usafiri toka sokoni hadi unapochomea~2,000-5,000 kutegemeana na umbali na aina ya usafiri.
Jumla ya msingi ni: 20,000+8,000+40,000+5,000=73,000/=(each maximized).
Kwa hiyo ukiwa na 100,000 unafanya biashara ya kupata 30,000 na zaidi daily.
 
Back
Top Bottom