Mary Abely
New Member
- Jun 15, 2023
- 4
- 4
UTANGULIZI
Biashara haramu ya usafirishaji binadamu ni kitendo cha kusafirisha binadamu kwa njia ya nguvu, tishio,kulazimishwa, kudangaywa au utekaji nyara kwa kusudi la dhuluma. Hujumuisha kuajiri kwa nyonya, kuhamisha, kusafirisha, kuhifadhi au kupokea watu. Lengo la biashara hii ni haramu ni unyanyasaji ikiwemo, kutumikishwa kingono, kazi au huduma ya kulazimishwa , kazi ya madawa ya kulevya, kuondolewa viungo muhimu kama figo na kadhalika kwa faida ya mtu mwengine.
( picha :eapcco.org/sw/ usafirishaji haramu wa binadamu).
Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina idadi kubwa ya wahanga watakanao na biashara haramu ya watu ndani ya mipaka ya Tanzania , hii hufanyika pale wasichana huchukuliwa kutoka vijiini kuletwa mjini kwa kufanya kazi ambazo ni za mateso ngumu, bila uhuru na malipo ni madogo kulinganisha na kazi wanzofanya. Pili , biashara hii hufanyika nje ya mipaka ya Tanzania. Biashara hii huwaathiri sana wasichana na watoto ikiwemo walemavu na vijana wenye nguvu.

Sababu za kukua kwa biashara haramu ya usafirishaji binadamu:
- Umasikini , na hali ngumu ya maisha ni moja ya sababu kubwa wasichana huchukua jukumu la kulea familia zao, hivyo hutafuta kazi mbali mbali ili waweze kupata kipato kitakacho saidia familia zao.Ndipo wanapokutana na janga la kunyonywa kimwili nakimaadili kwa faida ya watu wengine. watoto pia hasa walemavu kwamfano, imetambulika kuwa watoto husafirishwa kwenda nchini Kenya kwa lengo la kufanya kazi ya kuomba omba.
- Teknolojia, kupitia mitandao ya kijamii vijana wengi hushawishiwa na kulaghaiwa na watu walioko mijini na nje ya nchi. Vijana hundanganywa kulipwa pesa nyingi pindi waendapo mijini ama nje ya nchi kama DUbai . Hivyo hujikuta wakukumbana na ajira ambazo hawakuahidiwa kama biashara ya ndono na madawa ya kulevya ama mazingira magumu ya kutendea kazi. Kwa kuongezea hapa changamoto pia ya ajira nchini Tanzania hupelekea kukua na kuendelea kwa biashara haramu ya binadamu.
- kunyonywa na kunyanyaswa, watu waliosafirishwa, hususani wanawake na watoto' wanakumbwa na tatizo la kunywanyaswa kingono, hisia, kutumikishwa, na vitendo vingine ambavyo si vya kibinadamu.
- kudumaa kwa uchumi, usafirishaji wa binadamu kutoka sehemu moja kwenda nyingine hupunguza ngvu kazi ya nchi, kwasababu wahanga hawa hutolewa na kuwekwa mbali na elimu, ajira zenye tija na nafasi nyingine za uzalishaji katika nchi yao.
- kusambaa kwa magonjwa. usafirishaji haramu hupelekea kusambaa kwa magonjwa kama UKIMWI, kwa kukosa huduma za kiafya na hali mbaya ya mazingira wanayokumbana nao wahanga hao.
- Kupitisha sheria kali zinazolenga biashara haramu ya binadamu zikijumuisha kuwalinda wahanga na na msaada. Kuwapatia mafunzo na kuwajengea uwezo watekeleza sheria, majaji, na waendesha mashitaka katika kuchunguza na kutatua kesi za biashara haramu ya binadamu.
- Kuwapatia wanajamii elimu kama vile kuendesha kampeni za kuelimisha jamii kuhusu hatari itokanayo ni biashara haramu ya binadamu, viashiria na utaratibu wa kuripoti. Pia kuingiza elimu ya biashara ya binadamu katika mitaala ili kuongeza uelewa kwa wanafunzi.
- ushirikiano wa kimataifa, hii hujumuisha kupeana taarifa, kushirikiana na taasisi, nchi jirani na wadau mbalimbali jinsi ya kukabliliana na tatizo hili. Kuimarisha ulinzi mipakani na ushirikiano katika kuzuia usafirishaji wa wahanga nje ya mipaka.
- kupambana na umasikini na kuongeza fursa nyingi za kimaisha, Tanzania inapaswa kupambana na umasikini kwa kuanzisha programu tofauti tofauti kutatua sababu kuu ya biashara hii kama ukosefu wa ajira, elimu, na mzingira magumu ya kiuchumi. Kutengeneza fursa mbalimbali za kimaisha, programu za kuongeza ujuzi na kadhalika.
Kimataifa, watu milion 40.3 wao katika utumwa wa kisasa au wa kileo. biashara haramu ya kusafirisha binadamu bado ni uhalifu usio ripotiwa kwasababu hufanywa kwa usiri sana. Hivyo basi, ni jukumu letu watanzania kushirikiana na serikali kwa kutoa ripoti na taarifa pindi tunaoona tatitzo hili linajitokeza kwenye jamii zetu. Pia tuzijue haki zetu na kuheshimu haki za mtu mwengine tuache kutumikisha wengine kwa maslahi yetu binafsi, hii itasaidia kupunguza pia watoto wa mitaani ambao hutoka katika famila zao kwa lengo la kufanya kazi ya kuomba mijini na nje ya nchi. Natoa pia ushauri kwa vijana wanao kimbilia kazi nje ya nchi wakati hawana taarifa zaidi juu ya kazi na watu wanoenda kuwafanyia kazi.
Attachments
Upvote
2