TEMBO WANGU
JF-Expert Member
- Feb 21, 2014
- 930
- 1,290
Wakuu,kunabiashara ambayo wewe graduate unaona kama vile haikufai au huna mpango nayo, ni biashara ya video show, biashara hii inahitaji mtaji wa mchanganuo ufuatao, tv ya chogo inch 21@ 100000, deki samsug @50000, spika za uswazi@ 20000, kujenga banda la kuonyeshea@100000, kukodisha eneo la mwenye uwanja@15000*3=45000, hapo unakuwa umepata investiment capital sawa swa na 315000. kukodisha mikanda au CD za movi@500 kwa mikanda ya siku nzima ni mikanda 7, so kwa siku utatoa 3500, kama operation capital, CD moja ya movi unaweza ingiza 2000 au 3000, ukizidisha kwa CD 7; unauwakika wa kupata 15000, kwa siku,je wadau hapo ujaishi mjini kibishi, huku ukiendelea kuzunguka na bahasha kutafuta kazi. Apo ujaweka azam tv na DSTV,Unaweza kuboresha hiyo biashara kwa michango ya wadau wengine. Bongo akiri utaishi kwa amani.