Biashara hii inalipa pia wadau?

Biashara hii inalipa pia wadau?

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,290
Wakuu,kunabiashara ambayo wewe graduate unaona kama vile haikufai au huna mpango nayo, ni biashara ya video show, biashara hii inahitaji mtaji wa mchanganuo ufuatao, tv ya chogo inch 21@ 100000, deki samsug @50000, spika za uswazi@ 20000, kujenga banda la kuonyeshea@100000, kukodisha eneo la mwenye uwanja@15000*3=45000, hapo unakuwa umepata investiment capital sawa swa na 315000. kukodisha mikanda au CD za movi@500 kwa mikanda ya siku nzima ni mikanda 7, so kwa siku utatoa 3500, kama operation capital, CD moja ya movi unaweza ingiza 2000 au 3000, ukizidisha kwa CD 7; unauwakika wa kupata 15000, kwa siku,je wadau hapo ujaishi mjini kibishi, huku ukiendelea kuzunguka na bahasha kutafuta kazi. Apo ujaweka azam tv na DSTV,Unaweza kuboresha hiyo biashara kwa michango ya wadau wengine. Bongo akiri utaishi kwa amani.
 
Wadau hapo, ukiisimamia mwenyewe, mwanzo mwisho, na huku ukiweka DSTV NA AZAM TV, nakuhakikishia unaweza kutengeneza kipato cha kiaina kwa mwezi si chini ya laki tatu 300000; hapo kinachotakiwa ni kuondoa usharobaro au kujiona kuwa wewe ni msomi sana, kumbe kila siku unapiga mzinga wana wa buku mbili mbili, na hayo tu wadau.
 
Tembo wangu hili Bonge la Wazo aisee.
Kwa ufupi hulali Njaa.Nimeona jamaa wengi sana wanafanya hii kitu.

Huku Zanzibar kuna jamaa ameweka Pale Maeneo ya Magomeni,yaani ni mjini kabisaa,yaani anatumia uwani kwake.Basi watu kibaooo.

Kuna issue fulani za ajabu ajabu watu wanaziona lakini mwisho wa siku hesabu nzuri.
Kuna mama mmoja Chanika anaishi kwa Biashara hii na amefungua kiwanda cha Tofali kwa Biashara hii
 
Biashara za namna hii zinafaida kubwa Sana, cha muhimu Ni usiwe Na aibu ktka kutafuta.
 
ngoja maafisa vijana wa wilaya waje kufunga bibshara
 
Back
Top Bottom