Zillion
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 1,378
- 1,866
Shida yetu kubwa sisi watanzania hatuna elimu ya biashara
Uzi huu ni ushahidi tosha kuthibitisha hilo.
Ukitaka kuwa mfanyabiashara ni LAZIMA ujiulize haya maswali na upate majibu
1. Kwanini nataka kufanya biashara?
2. Nina ujuzi wa kutosha wa biashara ninayotaka kufanya?
3. Nina muda wa kusimamia biashara yangu/wazo langu?
4. Je Mimi ni mbunifu na niko tayari kukabiliana na changamoto ninazozijua na nisizozijua huko mbeleni?
5. Je mimi ni mwaminifu?
Biashara inahitaji muda kuliko pesa
Wale wanaotanguliza pesa kabla ya kutoa muda wao kujifunza na kuelewa vyema biashara husika huishia kupoteza.
Muda, ujuzi, uaminifu, nidhamu na uvumilivu ni mitaji mikubwa kuliko pesa kwenye biashara.
JIFUNZE KWANZA!