Biashara imenishinda, nimerudisha fremu ya watu

Biashara imenishinda, nimerudisha fremu ya watu

Boda boda hawa hawa wa mtaani ambaye anakaa wiki tatu bila kukuletea hesabu,,,,ukiwa nayo moja utaona ni rahisi ila ongezea mbili au tatu ndipo utaona mziki vijana wengi siyo waaminifu watakutia stress utauza boda zote vijana waaminifu ni mmoja kati ya kumi

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Mkuu mimi nina boda moja na chamoto nakiona yani mtu anakaa siku 5 bila tarifa bila hesabu ... hapa nlipo na tafta mtu mwaminifu ila sasa ntampa masharti makali kidgo
 
Hizi biashara bana, zinahitaji commitment ya hali ya juu sana, nawapongeza sana watu wote mliofanikiwa katika biashara.

Mimi sijui nilikosea wapi aisee, maana duka lilikuwa na mtaji wa around 10m, sasa hivi limebaki na 3.2m nimeamua kuuza bidhaa kwa bei ya jumla na kulifunga tu hilo duka, sitaki pressure tena.
Upo mkoa gani mkuu,mimi nije nichukue fremu ?
 
Kwa hiyo milion 10 ni mtaji mdogo? Kwa hiyo mtaji sahihi wa kuanzisha biashara ni shi ngapi?
Inategemea aina ya biashara,mfano biashara yenye faida ndogo km ya mahitaji ya nyumbani huo mtaji ni mdogo,lkn kwa biashara ya Chakula kwasababu ina faida kubwa huo mtaji ni mkubwa.
 
Tatizo watu muna dharau biashara ndogo ndogo ..mfano kuuza matunda kwa mtaji wa M4 tu ukosi Hadi 70k kila siku Kama Net Profit.
Nakubali mkuu, nina mdogo wangu alianza na matunda akawa anapiga faida ya maana tu, baada ya umaarufu akanza kutengeneza na fresh juices.

Sasahivi hakosi mpaka 1.5M-2M kwa mwezi, kaajiri watu kwasasa hashindi sana kazini na maisha saafi kabisa.

Hata yule MAK Juice ni mfano mwingind pia.
 
Acha masiara watu tuna mitaji ya laki tano familia zinaishi raha mstarehe na bia tunagonga na michepuko inakura bata
Biashara ya 500K inakufanya ule bata(starehe) yenye thamani gani?? Unajua watu mnayachukulia maisha simple sana, unless uwe na biashara ya genge la nyanya.

10M sio pesa ndogo, ila inapoingia kwenye biashara inaweza kuwa ndogo au isiwe kutokana na ana ya biashara.

Kwa biashara ya Hardware, Pharmacy, Spareparts za magari 10M ni kitu gani??

Na siku zote mtu anaidescribe fedha kutokana na mazingira yanayomzunguka, kwako nyingi kwa mwingine ni hela ya vacation.
 
Haikuwa na sababu ya kuikimbia hiyo biashara ingali hujui Nini kimekurudisha nyuma, Kama umedondoka bila kuangalia umejikwaa wapi amini nakuambia kuna hatari ya kujikwaa Tena na uanguke.
Kaa chini tafakari ni wapi umekosea kabla ya kuanza biashara nyingine maana inaweza kuwa njia ya kwenda kuzika hata hicho kidogo ulichobakiza.
Hata hao tunao waita successful business men walipitia hizi changamoto wengine hata kuanza upya (from zero) lakini baadae wakainuka Tena na hawakukubali kukata tamaa, sembuse ww ambaye unacho cha kuanzia.
Ushauri wangu usikate tamaa changamoto ni moja kati ya chachu ya kuyakaribia mafanikio, kikubwa ni jinsi utakavyozipokea hizo changamoto.
 
Mkuu Mtoto wa nzi mleta mada alikosea sana Frequent stock count kwenye biashara ya uchuuzi ni lazima, bila hvyo utafilisika tu!
Unajua katika Biashara tunazosisimamia ama kusimamiwa na ndugu zetu tuna Exempt sana Wage Bill, Time, Storage and Mostly we consider Transport coats of which is not the true cost of operation in Broad way.... Kuna namna nawaangaliaga Hawa Motivational Speakers nasema ... Hiiiiiii.... Sio kweli.... Kwa nafasi niliypo... Haina manufaa yoyote kuanzia TasafI mpaka hii ... UKINIPINGA NIJIE NA FACT SIO POYOYO..NIPO JIKONI....
 
Hizi biashara bana, zinahitaji commitment ya hali ya juu sana, nawapongeza sana watu wote mliofanikiwa katika biashara.

Mimi sijui nilikosea wapi aisee, maana duka lilikuwa na mtaji wa around 10m, sasa hivi limebaki na 3.2m nimeamua kuuza bidhaa kwa bei ya jumla na kulifunga tu hilo duka, sitaki pressure tena.
Bila kuloga biashara hutoboi
 
Shida Ni moja mnaofanikiwa kwenye biashara kipengele Cha ndumba mnagoma kuwaambia wenzenu..mnabaki tu biashara inahitaji nidham...shubamiti
 
Biashara ya 500K inakufanya ule bata(starehe) yenye thamani gani?? Unajua watu mnayachukulia maisha simple sana, unless uwe na biashara ya genge la nyanya.

10M sio pesa ndogo, ila inapoingia kwenye biashara inaweza kuwa ndogo au isiwe kutokana na ana ya biashara.

Kwa biashara ya Hardware, Pharmacy, Spareparts za magari 10M ni kitu gani??

Na siku zote mtu anaidescribe fedha kutokana na mazingira yanayomzunguka, kwako nyingi kwa mwingine ni hela ya vacation.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Jamii forum watu hawapo serious sikuhizi
 
Back
Top Bottom