Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Upo vizuri mkuu nimesoma kila kituo...wewe inaoneka ni mshauri wa biashara.
Mi nina tatizo natamani nilianzishie uzi japo watu watasema ni chai.naomba nishauri hapa hapa
Mkuu mimi biashara yangu nimeanza 2020 mwezi dec ndo mzigo wangu wa kwaza kuingia.
Ki ukweli sijawahi kopa nimekisanya mtaji kidogo kidogo.
Mpaka sasa hivi biashara mtaji wako sio mkubwa ila mzunguko ni mkubwa sana.
Yaani kwa wiki 1M kawaida inategemea na mzigo ulioko dukani.maana miziho inakuja na kuomdoka tatizo langu ni hivi
1.kwa kuwa bado nahitaji kukuza mtaji basi nimekua mtu wa mawazo na usingizi kukata yaani silali.mwanzo hapo kati hata jf nilikua siingii ila sasa hivi naingia kupoteza mawazo..
Yaani nawaza sana kuliko kipindi sina ela.yaani mawazo yangu nikiinza lki nataka laki mbil..yaani siridhiki..sion faida saa ingine
Swali langu hivi kuna siku utafanya biashara ufikie hatua relax kweli au ni mateso tu
2.hivi wafanya biashara wakubwa pesa zao wanaweka bank kwwli?
 
Thanks for the compliments bro, I appreciate and am happy that atleast nimekusaidia kupata mwanga wa ulicho hitaji in the first place.

Geita na Nyamongo somehow panahitaji 'muscles' kidogo kuliko Chunya esp. kwa mtu anayeanza na mwny mtaji mdogo. Lkn pia hizi sehem 2 km ulivosema hawa watu (wakurya & wasukuma) ni selfish sn na wametapakaa maeneo almost yote ya uchimbaji.

Huwa wanabebana kwa sababu zao na sometimes wanabaguana kwa sabab zao. Ila Chunya ni changanyikeni, jamii za kila aina zipo kule so unapata watu wengi 'wakuja' wa kufanya nao mishe ambao hawaangilii ethnicity mradi tu wanaona kuna fursa ya kufanikisha jambo lao.

Ushauri wangu; ukiwa tayar zama field, jifunze physically hata kama una hela behave in a way watu wasielewe, gap kubwa kati ya mchimbaji anayefanikiwa na asiyefanikiwa huwa ni right info na field experience, fedha huja kufanya execution tu kwa hyo km huna right info na experience nzur ya nn cha kufanya hela yako ama 'utapigwa' na matapeli au utaichannel in a wrong way.

Otherwise, km zilivyo field zingine, mining business inahitaji analysis ya kina, financial discipline, commitment na passion kwa kile unacho kifanya. Ni ngumu mwanzoni kwa kuwa haina matokeo ya haraka ama yanayoonekana ila in the longrun huwa inafanya vema sn so inahitaji patience sn huku ukimaintain focus ya unachotaka kuachieve.

All the best bro, [emoji120][emoji120].

Sent from my Nokia 1.3 using JamiiForums mobile app
 
Million 5 faida Kwa mwezi inatosha kabisa chamsingi. Chamsingi uendelee kujifunza kwenye hio biashara polepole itakuja kukyrengenezea hata million 7 Kwa mwezi inatosha hiyo
 
Utateseka mpaka uwe na biashara/mtaji/mzunguko kubwa kiasi cha kujilipa mamilioni kwa mwezi. Hata sasa hivi na biashara ndogo hakikisha unajilipa mshahara sio unachukua tu hela unapojisikia.
 
Wameshusha kutokana na janga la vita sio matajiri kuamishia mzigo huko maana vita ilipoanza tu nao wakapunguza interest zao, mbali na hivyo BOT &UTT wenyewe wanatamani elimu hii iwafikie wanachi wengi sema hata ikiwafikia bado ni kikwazo kwamaana bonds utazifurahia, ukiwa na mzigo mrefu hata ukiwa na mzigo mrefu pia kimbembe kipo kwenye kupata coupons hasa za BOT sio kitu rahisi kihivyo, mnada ukitangazwa watu wengi wanabid hii imepelekea washiriki wengi wanakosa, let's say serikali inataka kupata bl 20 tu lakini utakuta washiriki wanajitokeza kuikopesha serikali wanafikisha mtaji wa bl 100 wachache wanapata tena hao wachache utakuta wamebid kiasi kikubwa yaani wamenunua coupons kwa bei ya juu, all in all hata ukikosa mnada mwingine ukitangazwa unashiriki mpk unapata, ni muda mrefu bonds za BOT plus za UTT zimekuwa ni bonge moja la mchongo kwa waliosanukia mapema na ambao wanaoendelea kusanuka kwa maana sio kila mtu anamisuli ya kufanya biashara, faida yake ukiwekeza huko unapata faida bila misukosuko huku ukilinda mtaji wako, na kizuri zaidi serikali zote zinakopeshwa na wanachi wake sio Tanzania tu bali worldwide kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo bonds zitaendelea kuwepo tu.
 
Kwa hio hela nafikiri kama ungeiweka kwenye bonds ungeondokana na hizo headaches kabisa. Fanya 12%×300,000,000, hio ni uTT ila BoT wanatoaga hadi 15% at times.
Mkuu mara nyingi nimeona watu wakizungumzia hii bond za serikali,je hii imekaaje hiyo interest inalipwa kila mwaka au Kwa muda wote wa uwekezaji wako na je huwa ni Kwa muda gani?
Kwa sababu Kwa hesabu hapo ni 45m je ni kama Kwa mwaka ni sawa na 3.75 m Kwa mwezi which is good money Kabisa Tena bila hustles zozote
 
Utateseka mpaka uwe na biashara/mtaji/mzunguko kubwa kiasi cha kujilipa mamilioni kwa mwezi. Hata sasa hivi na biashara ndogo hakikisha unajilipa mshahara sio unachukua tu hela unapojisikia.
Yaani natesekaaa jamani..
Mmmh
Nilivyokua nakula mshahara nilikua na enjoy kuliko now
Hivi unatengenezaje formula ya kujilipa mshahara?
 
Niajiri mimi nikufanyie marketing ila mapenzi sipendagi napenda kazi .
Kama upo serious njoo pm nipo serious .
Hali sio mbaya kwako ila naweza kukusaidia ukapanda kidogo mshaara wangu ni 9 laki tisa
 
Na nimesikia rates za bot zitashuka hadi single digit, watu wanaacha kuzungusha pesa wanapeleka huko ili wafurahie maisha.
 
Mwekezaji utasemaje umewekeza mil 300 alafu faida mil 5 kwa mwezi alafu hapohapo unasema hujalipa wafanyakazi na gharama za kuendesha ofisi....FAIDA NI NINI?? Nadhani tatizo limeanzia hapo.
Hajakosea, kiswahili kinachanganya kwa english kuna profit na net profit, wewe unayoongelea ni net profit, ye kaongelea profit, si kitu cha kubishana ni kuelewa tu kamaanisha nn
 

Iam inboxing you.
 
Ukifikisha hio 1b hutakuwa na mawazo hayo vinginevyo the likes of Mo,SSB and co wangekuwa wanalala na kusafiri Tu. Utaweka kiasi huko kwenye bonds halafu utaendelea na mambo yaliyokupa hio 1b.
 
Ukifikisha hio 1b hutakuwa na mawazo hayo vinginevyo the likes of Mo,SSB and co wangekuwa wanalala na kusafiri Tu. Utaweka kiasi huko kwenye bonds halafu utaendelea na mambo yaliyokupa hio 1b.
Kweli mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…