Achukue baadhi ya hizi ....
1.Aje Dodoma afungue kiwanda cha kufyatua na kuuza tofali,hii biashara inalipa sana watu wanajenga balaa kwa Dodoma,hapa anaweza kuweka na ki min shop cha hard ware.location zipo nyingi sana za kufanya hii biashara.
2.Aje Dodoma afungue kiwanda kdg cha kusaga na kupaki unga wa mahindi,asee hapa pesa ataikimbia mahitaji ni makubwa sana,waliopo wanaofanya hii biashara hawakidhi mahitaji ya wateja kwamba mda mwingi unga haupo mitaani.location zipo za kutosha nawez kwemwelekeza bure kabisa.
3.Anunue tractor la kilimo alipeleke Manyara,hapa pesa ni nyingi sana na ya uhakika.location za kupeleka tractor kwa Manyara zipo nyingi sana na pesa zipo nyingi sana.