Biashara isiyo na mtaji iliyobadili maisha yangu

Mkuu Maisha ya Mtandaoni yana siri Kubwa sana........Usiwe unapenda kuingia ingia sana hasa hii Mitandao inayokutaka uweke Password yako au kuruhusu (Allow) jambo ambalo hukulitaka........!!!!!
tunadukuliwa
 
Humu ndani tumekuwa ni zaidi ya ndugu kutokana na wote kuwa na tatizo moja la kukosa ajira huku tukilalamikia kukosa mitaji lakini je unatambua kuwa unaweza usiwe na mtaji lakini ukaweza kujijengea chanell na kipato kikubwa na ukasahau kabisa kuajiriwa kama nilivyofanya mimi?

Mwaka 2012, nikiwa zangu home baada ya matokeo ya form 4,kutoka nikakutana na mzungu mmoja jina lake anaitwa Gennaro Barricelli, huwa bwana alikuwa ametokea Amsterdam ila katika maongezi nikashangaa akinambia kuwa hana nyumba wala sehemu ya kulala, basi nikajitolea nikampokea home nikawa nalala nae asubuhi tunaenda kutembea nikimuonesha maeneo mbali mbali ya jiji
katika maongezi yangu nikawa na lalamika sana kuhusu ajira huku nikiilalamikia malalamiko serikali.

Ndipo jamaa aliponielekeza fursa ambayo mpaka leo hii imenisaidia mengi na imenifanya nifahamiane na watu wengi sana duniani ishu yenyewe ni kupokea wageni mbali mbali kutoka nchi tofauti duniani (watalii), kwani wengi huwa hawajawahi kufika Tanzania hivyo hutafuta mwenyeji wa hapa Tanzania kwa ajili ya kuwatembeza sehemu mbali mbali pamoja na kuwapeleka kwenye vivutio mbali mbali kupitia site yao.

Basi akanielekeza nikajiunga na site hiyo, haikuwa ngumu kujiunga na ilikuwa ni rahisi sana. Basi nika seaech watalii ambao wanahitaji watu ambao wenyeji kwa ajili ya kuwatembeza kwa siku wakaazo kuwa Dar nikawapata
mara ya kwanza niliwapata 3, ambao walifikia gest ikawa asubuhi nawafata nawazungusha maeneo mbali mbali kama Zanzibar, Kilimanjaro, Tanga,
Bagamoyo na Dodoma kwa Tanzania gharama za safari pamoja na chakula walikuwa wanazilipa wao kama wao na siku wakiondoka nilikuwa naachia visenti kidogo mpka dola 1000, miatano.

Wale ambao nilikuwa nikiwapokea wakawa wanaenda kuelezea na wenzao na kunifanya nizidi kufahamiana na wengine zaidi, basi hali ikaendelea kuwa hivyo kiasi cha kupata wageni mpka 15kwa mwezi, wengine walikuwa wana hadhi mbali mbali kama wanafunzi, madaktari nk.
Nafasi za kujitolea
Natafuta kazi
Ukiwa muongo usiwe msahaulifu tafadhali
 
Kuwa tu Mmasai au funga rasta, utapata wabibi wa kizungu wa kumwaga.
 
Mmmmmmmh!

upload_2017-11-13_9-35-43.png
 
  • Thanks
Reactions: ovi
Mzungu (Mtalii) atoke huko kote hadi Tz pasipo kujua atafikia wapi???? Kwahiyo akalala ghetto kwako braza.... Chai na maharage kama kitafunwa sio poa kabisa chapati ingependeza zaidi.
 
Nenda znz utajionea

Mwaka Jana nilienda kumtafutia nyumba ya kupanga znz ndugu yangu mmoja ,.znz kuna flats national housing nyingi sasa wengi walikuwa wanatukatalia sabb wanawasubiria watalii wawapangishie kwa pesa ndefu vyumba 2 bafu,choo ndani self contain na kochi zipo ndani

Vijana wengi znz wana mchezo huo
 
Hakuna biashara isiyo na mtaji.

Mtaji wako wa kwanza ni muda. Umetumia muda mwingi kukaa na kutafuta watalii
Muda wa kusafiri nao huku na kule
Lazima ulijinunulia nguo, begi na vingine vingi kabla ya safari.
Elimu yako pia ni mtaji tosha.... kuongea kiswangilish hadi kuelewana nao si kazi ndogo
 
Humu ndani tumekuwa ni zaidi ya ndugu kutokana na wote kuwa na tatizo moja la kukosa ajira huku tukilalamikia kukosa mitaji lakini je unatambua kuwa unaweza usiwe na mtaji lakini ukaweza kujijengea chanell na kipato kikubwa na ukasahau kabisa kuajiriwa kama nilivyofanya mimi?

Mwaka 2012, nikiwa zangu home baada ya matokeo ya form 4,kutoka nikakutana na mzungu mmoja jina lake anaitwa Gennaro Barricelli, huwa bwana alikuwa ametokea Amsterdam ila katika maongezi nikashangaa akinambia kuwa hana nyumba wala sehemu ya kulala, basi nikajitolea nikampokea home nikawa nalala nae asubuhi tunaenda kutembea nikimuonesha maeneo mbali mbali ya jiji
katika maongezi yangu nikawa na lalamika sana kuhusu ajira huku nikiilalamikia malalamiko serikali.

Ndipo jamaa aliponielekeza fursa ambayo mpaka leo hii imenisaidia mengi na imenifanya nifahamiane na watu wengi sana duniani ishu yenyewe ni kupokea wageni mbali mbali kutoka nchi tofauti duniani (watalii), kwani wengi huwa hawajawahi kufika Tanzania hivyo hutafuta mwenyeji wa hapa Tanzania kwa ajili ya kuwatembeza sehemu mbali mbali pamoja na kuwapeleka kwenye vivutio mbali mbali kupitia site yao.

Basi akanielekeza nikajiunga na site hiyo, haikuwa ngumu kujiunga na ilikuwa ni rahisi sana. Basi nika seaech watalii ambao wanahitaji watu ambao wenyeji kwa ajili ya kuwatembeza kwa siku wakaazo kuwa Dar nikawapata
mara ya kwanza niliwapata 3, ambao walifikia gest ikawa asubuhi nawafata nawazungusha maeneo mbali mbali kama Zanzibar, Kilimanjaro, Tanga,
Bagamoyo na Dodoma kwa Tanzania gharama za safari pamoja na chakula walikuwa wanazilipa wao kama wao na siku wakiondoka nilikuwa naachia visenti kidogo mpka dola 1000, miatano.

Wale ambao nilikuwa nikiwapokea wakawa wanaenda kuelezea na wenzao na kunifanya nizidi kufahamiana na wengine zaidi, basi hali ikaendelea kuwa hivyo kiasi cha kupata wageni mpka 15kwa mwezi, wengine walikuwa wana hadhi mbali mbali kama wanafunzi, madaktari nk.
Acha porojo, kama hili ni jambo unaloona unahitaji kuchangia na watu basi ungeweka vielelezo vyote wazi, otherwise ungeweza kukaa kimywa tu

Na kama ndio mtego wa kupata pesa toka kwa wasio na ajira wenzio wakutafute uwatoze malipo ndio uwatajie hiyo site uliyojiunga, basi subiri mazumbukuku watakutafuta
 
Back
Top Bottom