Biashara itakayokupa faida ya bilioni 1 kwa mwaka

Biashara itakayokupa faida ya bilioni 1 kwa mwaka

Mwambie aingie mkataba na Diamond ili wapige show maana show moja ya Diamond kwa hapa bongo si chini ya milioni 100 ndani ya mwaka tayari
 
Ili utengeneza faida ya angalau bilioni moja kwa margin ya 2-7%inabidi uwekeze angalau mtaji wa 1 trilion au uwe na cash flow ya 5 trilion.Kwa hali y uchumi wa Tanzania biashra mpaka ifikie kiwango hicho unahitaji angalau 3 years.

Unaweza anza kwa kufikiri hivyo kisha ndo uende hatua inayofuata
Umeongea uhalisia mtupu,, hilo ni suala la kwanza,, lakini kufanikisha lile kilichopo kwenye makaratasi kuja kwenye uhalisia ni changamoto nyingine ngumu zaidi,,
 
Tatua moja kati ya hizi changamoto hapa ikiwa unahitaji biashara itakayodumu zaidi ya miaka 100. Suala la kuingiza 1B kwa mwaka itategemea na kiwango cha hela atakachowekeza. TIA

  1. NJAA
  2. UKOSEFU WA AJIRA
  3. MAGONJWA
  4. ELIMU
  5. UMEME/NISHATI
  6. UCHAFU
  7. USAFIRISHAJI
  8. MAKAZI
Ras wa Paroko ,Hizo ndio. Idea ,amalizie yeye mwenyewe na Wengine pia wamefaidika ,uliyeomba Idea Jiongeze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Kiwanda cha nguzo za zege awauzie tanesco, 2.biashara ya kuuza magari.
3. Biashara ya ujenzi wa nyumba bora za makazi na kuziuza kama wafantavyo nhc
4. Kampuni kubwa ya ujuenzi wa majengo, barabara, na madaraja
5. Kampuni kubwa ya ufugaji wa Kuku wa nyama na mayai na kilimo cha mazao kwa ajili ya kuuza nje ya nchi. Mkuu niunganishe na mzee tumpigie kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Billioni moja kwa mwaka ni pesa ndogo sana, issue ni kuwa na mtaji wa kutosha kufanya investiment kubwa na kuwa tayari kwa lolote. Mimi kwa experience yangu ya biashara ya famasi anaweza akafanya hivi (Theoretically):
Aanzishe reputable pharmacy chain ambapo kila mkoa atakuwa na famasi babkubwa za rejareja angalau 3; achague mikoa 30 tu ya Tanzania, hivyo jumla atakuwa na famasi 90. Kisha awe na famasi za jumla angalau moja Dar es salaam, Moja Arusha, Moja Mwanza na Moja Mbeya.

Famasi standard za rejareja = Millioni 30 kila moja; Famasi 90 => Billioni 2.7 a.k.a 2,700,000,000/=
Famasi standard za jumla = Millioni 150 kila moja; Famasi 4 => Millioni 600

Miezi sita ya mwanzo mfanye marketing na sales ya nguvu + grace period ya kuvumilia "ngombe wenu waanze kutoa maziwa ya kutosha"; baada ya hapo the rest is history!

Kila famasi moja ya rejareja itakupa faida (net profit) ya angalau Tsh 2,000,000/= kwa mwezi.
Famasi 90 x 2,000,000/= => 180,000,000/= kwa mwezi;
=> 180,000,000/= x 12 = 2,160,000,000/= kwa mwaka.

Kila famasi moja ya jumla itakupa faida (net profit) ya angalau Tsh 10,000,000/= kwa mwezi
Famasi 4 x 10,000,000/= => 40,000,000/= kwa mwezi;
=> 40,000,000/= x 12 = 480,000,000/= kwa mwaka.

Faida ya famasi za jumla + famasi za rejareja = 2,160,000,000/= + 480,000,000/=

= 2,640,000,000/= (Billioni Mbili na Millioni Mia Sita na Arobaini)

Ila ajiandae kwa kisukari, presha, kipandauso, kukosa usingizi, msongo wa mawazo, sonona na kadhalika.

NB:
- Huu sio ushauri wa kitaalam bali ni maoni ya kawaida, na ni nadharia tu kwa 100%; ukitaka kuwekeza ongea na wataalam wako wakushauri
- If you want to win big you gotta play big

Nawasilisha ........
Mkuu...[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Huu ufafanuz wako, kama ni mtindo wa ushonaji wa nguo basi unaiga kwa kuangalia umbo la nje bila kujua vipimo ni lazima utaharibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NB:
- Huu sio ushauri wa kitaalam bali ni maoni ya kawaida, na ni nadharia tu kwa 100%; ukitaka kuwekeza ongea na wataalam wako wakushauri
- If you want to win big you gotta play big

Nawasilisha ........

Aahahahahahahahahahaaaaa looh 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom