Issue ingeweza kuwa handled na TFF kwa sababu, kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, sio kwamba Biashara imekosa usafiri bali hakijapatikana kibali cha kutumia anga ya Sudan, nadhani na Libya or something like that!!
Utetezi waliotoa TFF ni kwamba wao walikuwa tayari kuwasaidia kuomba kibali cha kukatiza kwenye hizo anga lakini kwa bahati mbaya, nchi husika hazifanyi kazi Jmosi, na kwahiyo imeshindikana ombi lao la kukatiza kwenye anga zao kushughulikiwa!
The questions are:-
1. Nani ana wajibu wa kuomba vibali vya ndege kuruhusiwa kupita kwenye anga za nchi fulani...
2. Ilikuwajie vibali viombwe leo wakati safari ilifahamika tangu zamani.
3. Ina maana ATCL waliotaka kuwasafirisha Biashara hawakufahamu utaratibu wa kuomba vibali, au sio wajibu wao!!!
Ingawaje sifahamu majibu ya hayo maswali lakini TFF walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuhakikisha hayo hayatokei kwa sababu Biashara hawana uzoefu wa kukata mawimbi!!
Pale Biashara usishangae kukuta viongozi KARIBU wote ndo wameanza kupanda ndege mwaka huu walipoenda Djibouti... sasa ndo watafahamu taratibu za anga hawa!!