Salaam,
Kwanza, nimekuwa na uzoefu kwa muda juu ya biashara za China na Japan. Kwa mtaji wa 10mil ni kama nusu ya mtaji wa kuanzia kwa sababu kuna mambo matatu hapo. 1. Usafiri na malazi, 2. Ununuzi wa bidhaa na uhifadhi, 3. Upakiaji na Usafirishaji.
Biashara uliyopanga kuifanya naamini umeshafanya utafiti na kugundua ni nini kinachotakiwa. Unachopaswa kufanya kwa kuanza (kulingana na mtaji wako) tafuta wakala (online au wenye ofisi Tanzania) uweke order kulingana na mahitaji yako kisha mzigo ukifika unaanza kazi ya ku supply kwa hao wateja wako.
Ukifanya hivyo Mara nne au mara tano tayari utakuwa na uwezo wa kwenda mwenyewe na kujionea fursa zaidi za biashara nchini China. Sambamba na hilo nakushauri usiwekeze pesa yote kwenye mtaji wakati wa kuanza biashara hiyo kwa ajili ya dharura za kibiashara na wateja wako.