Nakumbuka kwenda huko na Visa nilinunua Online kwenye ukurasa wao wa Visa.
Nilinunua kama Mtanzania maana hadi leo bado Mtanzania ingawa Visa niliyonayo huenda ilinisaidia.
Ila ninavyofahamu kwenye swala la Visa, wanaangalia Passport yako na siyo Visa gani unayo.
Kila la kheri.
Nyongeza: Nilikuwa na fedha za kutosha kama wanavyodai uwe nazo yaani bajeti yako kwa siku. Sikumbuki ni ngapi ila nafikiri ukijiwekea Euro 100 kwa siku basi zinatosha. Ila kama utapata mwaliko, basi ina maana huyo mwenyeji wako ataonyesha kuwa ana fedha. Kama ni Kiwanda au kampuni, inaweza kuwa ngumu. Karibuni pia pande hizi kwa biashara.