Biashara kutoka Uturuki

Biashara kutoka Uturuki

Stuna,

Waturuki ndiyo biashara yao kubwa sana, ya nguo na wanazalisha pamba wenyewe. Niliona mashamba mengi tu huko kwao. Ila bei zao kidogo hawa jamaa huwa si nzuri. Kwa nchi za Ulaya, hasa Ulaya kati na magharibi, wengi wanaweza kununua nguo za hawa jamaa. Ila kwa Afrika, wachache.

Mturuki ana viwanda vingi mno na sababu kubwa ni ushirikiano wao na USA na ndiyo maana wapo kwenye umoja wa NATO. Usa amewekeza kwenye high tech na viwanda vya aina mbalimbali. Ukija kwenye mahoteli ndiyo usiseme, panafaa sana kwenda kula bata.
Kwa biashara Kama za nguo siwashauri Muende Turkey sababu ata wao utao China,nguo ni bei kule,mi uwa naendaga kula bata tu kila mwaka nitaenda tena January 2016
 
Wenzetu huwa hawataki kusema ila ukweli ni kuwa serikali inakuwa inajua kila kitu kuhusu wewe. Ukiwaficha, basi watasubiri wakati unafanya manunuzi. Ukiwa unanunua vitu vya bei mbaya na huna kazi, wanakutembelea.

Mara nyingi wanaangalia ulilipa kodi kiasi gani na hiyo inatumika kamamkigezo.

Kwan USA sifahamu utaratibu ukoje maana sijawahi kwenda. Lakini pia hata kama mtu hafanyi kazi ila Bank ana fedha za kutosha, basi hilo haliwi tatizo.

Ila ukweli ni kuwa kila nchi wana utaratibu wake, inabidi kusoma masharti yao ambayo mara nyingi yanakuwa yameandikwa wazi. Waturuki ni nchi ya kitalii, si wasumbufu sana na Visa yao ni Euro 15 tu kama sikosei. Ila USA wasumbufu sana na masharti mengi. Ila mwisho wa siku, hata huko, watu wanakwenda kila siku.

Mwenyeji anaonesha vipi kuwa ana fedha katika invitation letter kwa mtu binafsi(sio kampuni) na huo utaratibu wa kuonesha kiasi cha fedha upo hata kwa Marekani,maana kuna mtu anataka kuniandikia barua ya mwaliko lakini hajui vitu gani vya kuonesha,sasa hata kwenye fedha sidhani kama tunauelewa wa kutosha...kama unajua unaweza kutoa msaada pia hapa.

cc Money Stunna
 
Huku unańunua quality, quantityt zipo Asia. Kwa ufupi naweza kusema hivyo.

Hata vifaa vya Asia vinavyouzwa European Union, ni bora kuzidi vinavyouzwa Asia na Africa.

Kuna deal gani hasa huko za kibiashara kuliko ilivyo nchi za Asia kama Thailand na China hasa kwenye bei ya vitu.
 
Nakumbuka kwenda huko na Visa nilinunua Online kwenye ukurasa wao wa Visa.

Nilinunua kama Mtanzania maana hadi leo bado Mtanzania ingawa Visa niliyonayo huenda ilinisaidia.

Ila ninavyofahamu kwenye swala la Visa, wanaangalia Passport yako na siyo Visa gani unayo.

Kila la kheri.

Nyongeza: Nilikuwa na fedha za kutosha kama wanavyodai uwe nazo yaani bajeti yako kwa siku. Sikumbuki ni ngapi ila nafikiri ukijiwekea Euro 100 kwa siku basi zinatosha. Ila kama utapata mwaliko, basi ina maana huyo mwenyeji wako ataonyesha kuwa ana fedha. Kama ni Kiwanda au kampuni, inaweza kuwa ngumu. Karibuni pia pande hizi kwa biashara.

@ Steven, naona mada hii ni ya muda mrefu kidogo! Bado upo Poland?
Kama bado upo, mimi ningependa kujua kibiashara, ni products zipi kutoka UK zinahitajika huko?

Natanguliza shukran!
 
Back
Top Bottom