Pastor Achachanda
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 3,023
- 1,315
Wao hizo ndoo wanazifanyia nini noaja zina value kiasi hicho?
Mtu akiwa nazo ndani anaonekana ana maisha mazuri. Wanaweka maji na kutunzia bidhaa za mashambani. Pia wengine wanawindia wanyama kama sungura nk wakiweka chakula wakiingiza kichwa hawatoki. Pia kwa aliyeshangaa mayai 40 hicho ni kidogo mno. Mavago kuku ni wengi kama pikipiki za Mwanza au kule Songea hawaoni hasara kabisa. Pia wengi wamelala.
mkuu inamaana nikitaka kununua hao kuku?..yaani badala ya ndoo, niwape hela!
Ahsante sana
Kwa hela watakulalia. Zile ndoo ndogo zinauzwa tsh 2000. Wewe upate mayai 40 au kuku mzima ni veri bigi dil eva
Kama utakwenda Msumbiji fika kijiji cha Mavago jirani na Tunduru. Chukua ndoo za mafuta zilizotumika za kutosha. Kule hawatazinunua kwa hela ila mtabadilishana na kuku wa kienyeji wakubwa hujawahi kuwaona. Pia utaweza badilishana na mayai ya kienyeji. Mfano ndoo 1 ya lita kumi utaweza pata mayai 40 ya kuku wa kienyeji.
Hao ndugu wanaongea LUGHA gani, pia Km itawezekana unaweza kujua umbali wakutoka TUNDURU hadi hapo mavago? Gharama zikoje km hutajali,,,!
mkuu ile nchi ni ya watanzania, wako wengi kweli...si lilongwe wala mzuzu,ila kule vfaa vya ujenzi ni hela!
Pia kule baiskeli ni kama bodaboda au daladala
ukiuza vfaa vya baiskeli unaweza piga hela pia!
mkuu DZUDZUKU malawi kwenye suala la kilimo cha mazao ya chakula wako vizuri kwenye mahindi , maana ndio zao lao kuu la chakula
kwenye viungo vya chakula mfano nyanya , vitunguu maji/saumu nk hawalimi kwa wingi
tatizo kule ni thaman hela yao inashuka kila wiki, hii inaweza kuwa changamoto kwa biashara toka Nje, pia kule kuna mageti mengi hivyo ujiandae kwa ukaguzi wa mizigo na paspot barabarani
mkuu unawewza ukaenda na kufanya kautafiti kwani mimi nimeondoka huko mwaka juzi, hivyo kunaweza kuwa na mabadiriko ktk mambo mengi hasa baada ya kuingia kwa raisi mwanamke madarakani bi Joyce Banda
nisamehe mkuu sim yang ina uwezo mdogo wa kupost maneno mengi
kama kuna swali unaweza kuniuliza tafadhari!
Nashukuru kwa mchango wako, maana ndio nimeajiriwa sasa hvi huku Kyela nipo maeneo ya boda na Malawi, ninahitaji kufanya nao biashara, vp kuhusu biashara ya mazao kama mchele, mahindi, maharagwe, alizeti n.k?