Biashara ndo zinachangamoto hivi aisee? Msaada tafadhari

aBuwash

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2023
Posts
262
Reaction score
497
Mimi ni mfanya biashara mgeni kwenye nafaka sasa na leo ni siku ya pili kwenye hii biashara yangu.

Kasumba niliyokutana nayo wadau ni kwamba kuna mteja alikuja kununua mchele kilo 170 na unga ndogo tatu thamani ya shilling laki tatu na 87. Ile hela kanipa nimehesabu kwa macho yangu imetimia nikaweka mfukoni. Nikampakilia mzgo wake. Huyo mteja anatokea chamanzi kwa maelezo yake. Basi kashaondoka nahesabu tena ile hela nakuta ni laki moja na elfu kumi yanii laki mbilii na 77 haipo.

Dah wenye uzoefu wanifafanulia jamaa katumia njia ipi kuniibia hela nyingi kiasi kile na mimi mwenyewe hata sikushtuka hivi huwa wanatumia dawa hawa matapelii msaada please? kama imewahi kukutokea naomba experience yako hapa.
 
Huyo alitumia chuma ulete Sasa Ili kuepuka Hilo tatizo lisijirudie Tena fanya yafuatayo:
✓Mtangulize mungu Kila unapofungua biashara yako pamoja na kufunga.
✓Sehemu ambayo unaweka pesa Aidha ya mauzo au akiba yako hakikisha umeweka punje za kitunguu swaum kilichomenywa kuanzia mbili na kuendelea.
✓weka mkaa pia kwenye pesa za mauzo au akiba
✓weka ndulele wengine huita mtula tula kwenye hizo pesa zako za mauzo.
NB:
Itapebdeza sana kama ukipata vitu vyote hivyo tajwa hapo juu na ukavichanganya kwa pamoja.
 
Pole sana. Kwenye fedha yako ya mauzo weka mkaa na vitunguu swaumu vilivyomenywa
 
Mungu anasaidiwa na uchawi? Anyways, hakuna kitu kama chuma ulete, hii ni imani ya kijinga kabisa. Sana sana ni matapeli tu wanakuchota na maneno tu.
 
Hoja ya msingi ipo hapo kwenye bold,labda kama ”mungu” lakini kama ni ”Mungu" hivyo vingine ulivyoorodhesha hapo havihitajiki.

Mleta mada kuwa na utaratibu baada ya kumuuzia mteja mzigo pesa zake usizichanganye na nyingine (unaweza ukazifunga na rubber band kuzitenga na nyingine) hii itajenga kumbukumbu zako vizuri zaidi kwamba hela fulani ilikuwa hivi na hata ikitokea umeitumia ni rahisi kukumbuka,labda ulipopokea hiyo hela kuna malipo ulifanya ndiyo maana hesabu zimepotea.
 
Hesabu vizuri pesa zako next time chuma ulete ingekuwa dili hakuna mkoa ungekuwa na matajiri kuwazidi sumbawanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…