Biashara ndo zinachangamoto hivi aisee? Msaada tafadhari

Inaonekana bado unaishi kwa shemeji au umeandika kiutani
Na ukitaka kuamini hii mbinu mfanyie mtu unayefamiana nae utakuja kunipa majibu..wafanya biashara wengi wenye wenge huwa wanapigwa kwa style hii.kwa kuwa hawanampango wa kuhakikisha malipo mara mbili.
 
Kwelii mzeee wewe umenena kwaiyo nini kifanyike
 
ndo unakomaa hapo sasa kwenye biashara
 
Inaitwa 'chenjikota!'

Kuamini uchawi/ chumaulete ni ubwege wa hali ya juu.
 
Kwelii mzeee wewe umenena kwaiyo nini kifanyike
Chakufanya ni kuondoa wenge la mauzo kwenye biashara,mteja akikupa hela hakikisha hazirudi kwake mpaka mtakapokubaliana kuwa hakuna biashara baina yenu itakayofanyika..kinyume na hapo utalia Daily
 
Hapo umetapeliwa ulipewa hela kamili 387,000 ukahesabu kuna namna lazima alikuzubaisha ukairudisha ile hela sasa hapa akakupa 112,000 hiyo iliyokunjwa kifundi ikiwa na buku mbili mbili nyingi kwa kua uliisha hesabu akili itakuambia ni pesa ile ile ukatupia kwenye droo,
Ukamfungia mzigo akatembea.
 
Kweli kabisa mara ya pili sikuhesabu tena nilichogundua ni kuhesabu hela mara mbili mbili
 
Kweli kabisa mara ya pili sikuhesabu tena nilichogundua ni kuhesabu hela mara mbili mbili
Kwa hiyo ni kweli unathibitisha kwamba alivyokulipa hela kwa mara ya kwanza ukamrudishia hela kisha baadae akakulipa tena?kama ni hivyo hakuna chuma ulete hapo alikuzidi ujanja tu wa kukuzubaisha
 
Kwa hiyo ni kweli unathibitisha kwamba alivyokulipa hela kwa mara ya kwanza ukamrudishia hela kisha baadae akakulipa tena?kama ni hivyo hakuna chuma ulete hapo alikuzidi ujanja tu wa kukuzubaisha
Mtoa mada ndicho alichofanyiwa huwa wana Target Biashara mpya na kwenye huduma za uwakala pia. Pesa ukipokea kwa mteja huwa hairudishwi ni either achukue alichonunua au aondoke mkianza kurudishiana pesa kuna mianya ya utapeli au kupeqa Pesa feki.
 
Sasa kama haijatimia unafanyaje na unamwambia haijatimia anakwambia lete tuhesabu
 
HIVI HAWA MBUZI WANAOSEMA HAKUNA CHUMA ULETE WALISHAWAI FANYA HATA YA KUUZA MKAA??? HIVI HAWA JAMAAA WANAJUA ULIMWENGU ULIVYO KATIKA SEHEMU ZA BIASHARA ??? CHUMA ULETE IPO WAZEEE NA NI REAL KABISA TENA SIKU HIZI IPO ADVANCED KABISA UNAWEZA UKAPEWA BUKU NA UKARUDISHA CHENCHI ZA KUTOSHA

CHUMA ULETE NI UCHAWI TU NYIE VIJANA ACHENI KUONA WATU WAJINGA ETI HAWAKO MAKINI KATIKA KUHESABU HELA.!

NA UTAPELI PIA UPO KTK BIASHARA KUNA KUZIDIA MBINU NA MATAPELI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…